Rais Kenyatta kufungua kiwanda cha kutengeneza Meli Kisumu

Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumanne atafungua rasmi kiwanda cha kutengeneza na kukarabati meli kilichoundwa na vikosi vya ulinzi hapa nchini KDF, katika kaunti ya Kisumu.

Rais pia atashuhudia shughuli ya kuele majini Meli ya MV Uhuru II, ambayo ni ya kwanza kabisa kutengenezewa hapa nchini tangu mwaka 1966.

Also Read
Si shangwe kwa wamiliki baa, muda wa kuhudumu utaendelea kutekelezwa

Kiwanda cha kutengeneza na kukarabati meli cha Kisumu, ni kampuni iliyo chini ya wizara ya Ulinzi, iliyojukumiwa kuongoza na kuchochea utengenezaji wa Meli katika kanda ya Afrika Mashariki.

Also Read
Mudavadi atoa wito wa mdahalo wa kitaifa kuhusu mswada wa BBI

Vikosi vya ulinzi hapa nchini KDF, vilianzisha ujenzi wa kiwanda hicho kipya cha kutengeneza na kukarabati Meli, kama sehemu ya kupanua uchukuzi wa majini.

Also Read
KBC kushirikiana na EAC katika matangazo ya moja kwa moja

Ukarabati wa bandari ya Kisumu kuifanya kuwa kituo cha kisasa cha safari za majini, ulilenga kuboresha uwezo wake wa kushughulikia vyombo vikubwa vya majini kutoka Kenya hadi katika masoko ya Afrika Mashariki.

  

Latest posts

Wateja Milioni nne wa Fuliza kuondolewa kutoka CRB

Tom Mathinji

Watu watatu wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Rais Ruto: Serikali kudhibiti vilivyo makali ya njaa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi