Rais Kenyatta: Mataifa ya Afrika Sharti yakabiliane kikamilifu na zimwi la Ufisadi

Rais Uhuru Kenyatta amesema mataifa ya bara Afrika yanafaa kuwekeza katika vita dhidi ya ufisadi na uhalifu kati ya mataifa mbali mbali kwa sababu bara hili hupoteza takriban dola bilioni 88.8 kila mwaka kupitia vitendo vya uhalifu.

Rais alisema hasara hiyo ni sawia na asilimia 3.7 ya pato jumla la bara Afrika. Akiongea katika kaunti ya Mombasa baada ya kufungua rasmi kongamano la nne la kanda hii la chama cha kimataifa cha viongozi wa mashtaka (IAP), na chama cha viongozi wa mashtaka katika kanda ya Afrika Mashariki (EAAP), Rais alisema changamoto kubwa zaidi katika vita dhidi ya uovu huo ni hali ya bara hili kushindwa kutekeleza haki kwa haraka.

Also Read
Shughuli za uvuvi katika Ziwa Naivasha huenda zikasambaratika kutokana na uvuvi haramu
Also Read
Waziri wa kigeni wa China kufanya ziara ya siku mbili nchini Kenya

Aliongeza kuwa Kenya imeendelea kuongeza mgao wa bajeti kufadhili mfumo wa haki na inatumia mbinu ya mashirika mbali mbali ya kukabiliana na uhalifu unaohusisha mataifa mbali mbali.

Aliwahimiza wadau kubuni sera na kuafikia maazimio ya kukabiliana ipasavyo na ugaidi, ulanguzi wa mihadarati, ufisadi, ulanguzi wa pesa, masuala ya wanyama pori na mali ya kitamaduni.

Also Read
Wakenya wengi wana imani na tume ya IEBC kuandaa uchaguzi huru na haki

Kongamano hilo linawaleta pamoja wanasheria wakuu, maafisa wakuu wa mashtaka na wakurugenzi wa mashtaka ya umma kutoka kote duniani na hutoa fursa ya kubadilishana mawazo katika sekta ya haki.

  

Latest posts

Shikanda ahifadhi uenyekiti wa AFC Leopards

Dismas Otuke

Kalle Rovanpera atwaa ubingwa wa raundi ya Kenya mashindano ya WRC

Tom Mathinji

Ajali ya kwanza yatokea katika barabara ya Expressway

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi