Rais Kenyatta na Mama Taifa Margaret Kenyatta wachanjwa dhidi ya Covid-19

Rais Uhuru Kenyatta, mama wa taifa Bi. Margaret Kenyatta, na waziri wa afya Mutahi Kagwe wamechanjwa dozi ya kwanza ya chanjo dhidi ya virusi vya corona huku wakilenga kuwahakikishia wananchi kuhusu usalama wa chanjo hiyo.

Walipokea chanjo hiyo baada ya Rais kutoa wito kwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 58 kujitokeza kupewa chanjo hiyo.

Also Read
Wanasayansi chipukizi nchini watakiwa kutumia ujuzi wao ipasavyo

Katika hotuba yake kwa taifa, Rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa kiwango cha maambukizi ya virusi vya corona cha asilimia 22 kinatisha, huku taifa hili likinakili kiwango cha juu cha vifo cha watu saba kila siku katika mwezi wa Machi.

Kiwango hicho ni cha juu zaidi tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza cha Covid 19 mwezi Machi mwaka uliopita.

Also Read
Kenya yaorodheshwa nambari tatu Barani Afrika inayopokea pesa nyingi zaidi kutoka ng’ambo

Serikali imenunua chanjo ya Oxford-AstraZeneca lakini kumekuwa na wasiwasi kuhusu chanjo hiyo huku watu wachache wakijitokeza kuchanjwa.

Wakenya wameelezea wasiwasi kuhusu chanjo hiyo hasa baada ya kuibuka kwa ripoti kuhusu usalama wake.

Serikali ilinunua dozi milioni 1.02 ya chanjo hiyo ya Oxford-AstraZeneca huku wafanyikazi wa mstari wa mbele wa afya, walimu na maafisa wa usalama kote nchini wakilengwa kuchanjwa.

Also Read
Uhuru Kenyatta: Ushirikiano wa Kimataifa ni muhimu ili kutatua changamoto za dunia

Taifa hili linatarajiwa kupokea dozi nyingine milioni 24 za chanjo hiyo mwezi ujao.

Mapema juma hili chama cha madaktari cha KMPDU, kiliidhinisha uzinduzi na utoaji wa chanjo hiyo huku kikisema kuwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona linatatiza utendaji kazi na kuathiri rasilmali chache zilizoko za sekta ya afya nchini.

  

Latest posts

John Nkengasong: Omicron sio virusi vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi milioni 2 za chanjo aina ya AstraZeneca kutoka Ujerumani

Tom Mathinji

Watu 96 zaidi waambukizwa COVID-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi