Rais Kenyatta: Serikali imejitolea kuboresha mpango wa afya kwa Wote

Serikali imekariri kujitolea kwake kutoa huduma bora na za gharama nafuu za afya kwa raia wake kwa kuongeza vishawishi zaidi kwa ule mpango wa afya kwa wote.

Akiongea Jumamosi katika kaunti ya Mombasa wakati wa uzinduzi wa usajili wa kielektroniki wa wasiojimudu katika jamii kwenye mpango huo, rais Kenyatta aliziagiza wizara za afya na leba kuanzisha mara moja zoezi hilo la kuwatambua na kuwasajili wasiojimudu kwenye mpango huo.  

Akieleza imani yake kwa uwezo wa nchi hii wa kufankisha mpango wa afya kwa wote, rais Kenyatta alilihimiza bunge kuharakisha kupitisha sheria zinazohitajika ili kuutekeleza mpango huo kikamilifu.

Also Read
Rais Kenyatta afungua kampuni ya kutengeneza Meli Kisumu
Also Read
Idadi ya maambukizi ya COVID-19 yafika 83,316 baada ya watu wengine 711 kuambukizwa

Alisema hakuna Mkenya anayepaswa kuondoka humu nchini kwenda nje kupokea matibabu ambayo wanahitaji.

Rais Kenyatta alitoa onyo kali kwa walaghai katika sekta ya afya, akihimiza kuharakishwa mfumo wa kielektroniki wa ununuzi bidhaa katika halmashauri ya usambazaji dawa nchini-KEMSA, hazina ya  taifa ya bima ya matibabu-NHIF na wizara ya afya.

Also Read
Maduka 185 ya kuuza dawa yafungwa kwa kukiuka sheria

“Yeyote atakayejaribu kuilaghai hazina ya NHIF atachukuliwa hatua kali za kuambatana na sheria,” alisema raia

Waziri wa afya kwa upande wake, alielezea kujitolea kwa wizara hiyo kuhakikisha mpango huo wa afya unafaulu.

  

Latest posts

Familia ya Mbijiwe yatoa wito kwa Rais Ruto kusaidia kumpata mwana wao

Tom Mathinji

Uchukuzi kutatizwa katika barabara ya Lang’ata mwishoni mwa Wiki

Tom Mathinji

Kaunti za Isiolo na Siaya zamulikwa kwa ufujaji wa fedha

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi