Rais Museveni awaomba Wakenya msamaha

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewaomba msamaha wakenya pamoja na Rais Dkt. William Ruto kuhusiana na jumbe za kejeli katika mtandao wa kijamii wa tweeter, zilizotumwa na mwanawe jenerali Muhoozi Kainerugaba dhidi ya Kenya.

“Pole sana ndugu zetu Wakenya. Pia  pole kwa raia wa Uganda ambao huenda walikasirishwa na mmoja wa maafisa wa nchi hiyo,” alisema Museveni.

Also Read
Bobi Wine sasa adai maisha yake yamo hatarini

Katika taarifa, Rais Museveni alisema ni hatia kwa maafisa wa umma, wawe raia au wa kijeshi kuingilia maswala ya ndani ya nchi jirani.

Huku akiwapongeza raia wa kenya kwa kuendesha Uchaguzi Mkuu wa amani mnamo tarehe tisa mwezi Agosti mwaka huu, kiongozi huyo wa muda mrefu wa Uganda, alimpongeza Rais Dkt. William Ruto kwa ushindi wake.

Also Read
Wakenya waonywa dhidi ya kutoa jumbe za kupotosha

Museveni kupitia taarifa alisema amezungumza binafsi na Rais William Ruto kuhusiana na suala hilo.

Museveni alisema  kamanda huyo wa zamani wa majeshi ya nchi kavu alikosea kwa  kuingilia masuala ya ndani ya Kenya.

Alisema nchi zenye uhusiano bora hutangamana kupitia muungano wa mataifa ya bara Afrika ama kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Also Read
Mahakama yasimamisha utoaji chanjo kwa watoto dhidi ya Covid-19

Alisema uamuzi wa kumpa madaraka Muhoozi ni kutokana na mchango wake nchini humo, ambao usingevurugwa na tukio la ukosefu wa heshima alioonesha.

Aidha Museveni aliwaomba msamaha raia wa nchi hiyo ambao huenda walighadhabishwa kutokana na jumbe hizo za twita.

  

Latest posts

Wabunge wa Kenya wawakwatua Wabunge wa Tanzania mabao 3-1

Dismas Otuke

EACC kutwaa Mali ya shilingi Milioni 216 ya afisa mmoja wa kampuni ya KETRACO

Tom Mathinji

Gavana Waiguru awaalika Wawekezaji katika Kaunti ya Kirinyaga

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi