Rais Samia Suluhu Hassan afanya mabadiliko katika baraza la Mawaziri

Rais Samia Suluhu wa Tanzania amefutilia mbali uteuzi wa mawaziri watano na kumteua mkuu mpya wa sheria.

Mawaziri waliotimuliwa ni pamoja na Faustine Ndugulile waziri wa mawasiliano, Leonard Chamuriho waziri wa uchukuzi na Medard Kalemani waziri wa kawi.

Rais Suluhu pia alimteua upya January Makamba ambaye uteuzi wake ulikuwa umefutiliwa mbali na aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo hayati John Magufuli.

Also Read
Misri yagadhabika huku Ethiopia ikianza kujaza maji tena bwawa lake kubwa kwenye Mto Naili

Makamba sasa atahudumu kama waziri wa kawi. Wizara ya ulinzi iliyokuwa ikiongozwa na marehemu Elias Kwandikwa aliyeaga dunia mwezi agosti sasa inaongozwa na Stergomena Tax ambaye anakuwa mwanamke wa kwanza kushikiliwa wadhifa huo nchini humo.

Also Read
Ngozi Okonjo-Iweala kuwa Mwafrika wa kwanza kuongoza WTO

Rais Suluhu pia alimteua jaji Eliezer Feleshi kuwa mkuu mpya wa sheria kuchukua mahala pa Adelardus Kilangi ambaye sasa ameteuliwa kuwa balozi.

Dkt. Feleshi kabla ya kuteuliwa kwake katika wadhifa huo mpya, alikuwa Rais wa mahakama kuu ya nchi hiyo.

Also Read
Ufaransa yashauriwa kuchukua hatua zaidi ili kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya COVID-19

Kulingana na taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa mawasiliano ya RaisĀ  Jaffar Haniu, mwanasheria mkuu huyo mpya na Mawaziri hao wapya, wataapishwa Jumatatu tarehe 13 katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.

  

Latest posts

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Ethiopia yakaribisha wito wa kurejelewa mazungumzo na majirani wake kuhusu bwawa katika mto Nile

Tom Mathinji

Bwawa katika mto Nile lazidisha uhasama kati ya Ethiopia, Sudan na Misri

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi