Rais Uhuru Kenyatta awaalika wawekezaji wa Uingereza humu nchini

Rais Uhuru Kenyatta amewaalika wawekezaji wa Uingereza kutumia fursa ya nafasi za kibiashara zilizoko humu nchini, akisema nchi hii ingali kitovu cha uwekezaji barani Afrika.

Rais aliangazia fursa kumi za uwekezaji wa thamani ya dolla bilioni tano ambazo zinapatikana humu nchini.

Also Read
Messi akubali kusalia Barcelona baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitano

Fursa hizo ni pamoja na mradi wa kuweka taa jijini Nairobi, mfumo wa uchukuzi wa kasi wa mabasi jijini, Mradi wa kijasusi wa usimamizi wa trafiki na mradi wa kilimo cha unyunyiziaji mashamba maji wa Galana Kulalu miongoni mwa miradi mingine.

Also Read
KCAA yasimamisha safari za ndege kati ya Kenya na Somalia

Kiongozi wa nchi alitoa mwaliko huo wakati wa kongamano la kibiashara lililoandaliwa na waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza Dominic Raab na meya wa jiji la London William Russell, katika makazi rasmi ya Meya.

Also Read
Baraza la Magavana laidai hazina kuu shilingi bilioni 66

Wakati wa hafla hiyo, waziri wa mashauri ya kigeni Dominic Raab, alitangaza uwekezaji mpya wa shilingi bilioni 20 kutoka serikali ya Uingereza na uwekezaji wa kibinafsi kwa miradi minne mikubwa ikiwemo ile ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu na utengenezaji bidhaa.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Mzozo wa kidiplomasia kati ya Uchina na nchi za magharibi wasitishwa

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi