Rais wa Ivory Coast na mpinzani wake wakutana kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara alikutana na mtangulizi wake aliyepia mpinzani wake Laurent Gbagbo tangu kuzuka kwa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Ghasia hizo ambazo zilisababisha watu 3,000 kuaga dunia, zilizuka baada ya Gbagbo kudinda kukubali kushindwa katika uchaguzi huo mkuu.

Kiongozi huyo wa zamani wa Ivory Coast alirejea nchini humo mwezi uliopita baada ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC kumwondelea mashtaka dhidi ya uhalifu wa kibinadamu. Viongozi hao wawili wamekuwa wakishinikisha kuwpo amani na upatanisho.

Rais Alassane Ouattara alimkaribisha mtangulizi wake Gbagbo katika ikulu ya Rais jijini Abidjan siku ya Jumanne. Picha kutoka kwa mkutano huo zilionyesha viongozi hao wawili wakitabasamu na kushikana mikono.

Gbagbo alitoa wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wote waliowekwa kizuizini tangu kuanza kwa vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe.

Gbagbo alitiwa nguvuni akiwa katika ikulu ya Rais mwezi Aprili mwaka 2011 na kupelekwa katika mahakama ya ICC jijini Hague. Baada ya kuondolewa mashtaka dhidi yake na mahakama hiyo, aliishi katika jiji kuu la Ubelgiji,kabla ya kualikwa kurejea nyumbani na Rais Ouattara.

Gbagbo alirejea nchini humo mwezi jana na kulakiwa na wafuasi. Hata hivyo anakabiliwa na kifungo cha gerezani cha miaka 20 baada ya kuhukumiwa bila yeye kuwepo kwa wizi wa benki moja wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Na BBC

  

Latest posts

Mauaji ya mwanaume mmoja yazidisha taharuki Ol Moran

Tom Mathinji

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

IEBC kuongeza Idadi ya nchi za ugenini ambako wakenya watashiriki kwa upigaji kura

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi