Rais wa Muungano wa Milki za Kiarabu Sheikh Khalifa amefariki

Rais wa muungano wa milki za Kiarabu  Sheikh Khalifa bin Zayed al-Nahyan, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73.

Sheikh Khalifa ambaye alitawala muungano wa UAE tangu mwaka 2004 aliugua ugonjwa wa kiharusi tangu mwaka 2014.

Also Read
China kutoa mikopo ili kuweka 'mtego wa madeni’ kwa Afrika ni kauli za uzushi tu

Tangu alipougua ugonjwa huo wa kiharusi, Sheikh Khalifa, hakuonekana hadharani, lakini aliendelea kutekeleza majukumu yake.

Licha ya kuwa Rais wa muungano wa milki za Kiarabu, Sheikh Khalifa alikuwa kiongozi Abu Dhabi, ambao ndio mji mkuu wa milki saba zinazojumuisha muungano wa UAE na ambao una utajiri mkubwa wa mafuta

Also Read
Watu 26 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Majukumu ya marehemu Sheikh Khalifa bin Zayed al-Nahyan sasa yanatekelezwa na ndugu yake Mohamed bin Zayed al-Nahyan.

Also Read
Rais Kenyatta amuomboleza Rais wa Milki za Kiarabu marehemu Sheikh Khalifa

Kutokana na kifo cha Rais huyo, wizara ya maswala ya Rais imetangaza siku 40 za maombolezi, huku bendera zote zikipeperushwa nusu mlingoti kuanzia siku ya Ijumaa.

  

Latest posts

Serikali ya Uingereza yaidhinisha uuzaji wa klabu ya Chelsea kwa pauni bilioni 4 nukta 25

Dismas Otuke

Wahasibu watakiwa kufichua ufisadi bila uwoga

Tom Mathinji

Waakilishi wa Kenya ,Prisons na KCB wasajili ushindi wa pili mashindano Afrika kwa Voliboli ya vidosho

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi