Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir avunja bunge la nchi hiyo

Rais wa Sudan kusini Salva Kiir amevunja bunge na kutoa nafasi ya kuteuliwa kwa wabunge kutoka pande pinzani katika mkataba wa miaka mitano wa kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe. 

Wanaharakati na makundi ya kijamii wamesema kuwa hatua hiyo ilikuwa imechelewa kutekelezwa.

Mkataba wa amani uliotiwa saini miaka mitatu iliyopita uliamua takriban robo ya wabunge wangetoka katika chama cha mpinzani wa  Kiir, Riek Machar.

Wengi wa wabunge  550 watatoka katika chama tawala cha  SPLM.

Wabunge wa Sudan kusini hawatachaguliwa bali watateuliwa na vyama mbalimbali vya kisiasa.

Mzozo ulizuka nchini Sudan kusini mwaka wa 2013 na ukasababisha mzozo mkubwa zaidi wa kibinadamu huku watu wapatao elfu 380 wakiuawa na mamilioni ya wengine wakilazimika kutoroka makazi yao.

Serikali ya umoja imekuwepo kwa zaidi ya mwaka mmoja, lakini kufuatia kuzuka kwa mzozo wa kikabila Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu hatari ya kutokea tena kwa mzozo mkubwa nchini Sudan Kusini.

  

Latest posts

Mwanaume mmoja ashtakiwa kwa makosa saba ya mauaji Marekani

Tom Mathinji

Uganda yaidhinisha Kiswahili kuwa Lugha rasmi

Tom Mathinji

Walinda usalama wawili wa Umoja wa Mataifa wauawa nchini Mali

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi