Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemshtumu mbunge mmoja kutoka chama chake tawala ambaye anajulikana kwa kupinga chanjo dhidi ya maradhi ya Covid-19.
Josephat Gwajima, mbunge wa eneobunge la Kawe ambaye pia ni mhubiri mwenye wafuasi wengi mtandaoni, amekuwa akipinga chanjo dhidi ya maradhi ya Covid-19 akisema bila ushahidi kuwa chanjo hizo sio salama na Watanzania wanapaswa kuzikataa.
Hivi karibuni, mbunge huyo, aliishtumiwa bungeni kwa maoni yake. Swala la chanjo limekuwa nyeti kisiasa nchini Tanzania, kutokana na maoni ya marehemu Rais John Magufuli ambaye alitilia shaka uwepo wa maradhi hayo.
Samia ambaye ni Rais mpya amebadilisha sera ya marehemu magufuli na kuzindua utoaji wa chanjo.
Hivi karibuni mbunge huyo amechukuliwa hatua na bunge kwa sababu yakauli zake hizo