Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aambukizwa Corona

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amethibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19.

Hii ni kulingana na taarifa rasmi kutoka kwa afisi ya Rais huyo.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 42 alipimwa baada ya kudhihirisha dalili za kwanza za ugonjwa huo na kwa sasa amejitenga kwa siku saba.

Also Read
Mwaniaji urais nchini Uganda 'Bobi Wine' aachliwa huru kwa dhamana

Hata hivyo Macron ataendelea kutekeleza majukumu yake kama rais kutoka mahali atakapouguzwa hadi atakapopata nafuu.

Haijabainika jinsi Macron alivyoambukizwa ugonjwa huo, huku afisi yake ikiwa imeanzisha uchunguzi kuhusu watu waliokaribiana na rais huyo.

Also Read
Israeli yaonya kuhusu ufaafu wa Rais Mteule wa Iran Ebrahim Raisi

Taifa la Ufaransa lilitangaza amri ya kutotoka nje mapema wiki hii ili kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya ugonjwa huo.

Ufaransa imeripoti zaidi ya visa milioni mbili vya maambukizi ya COVID-19 tangu kuanza kwa janga hilo huku zaidi ya wagonjwa 59,400 wakiaga dunia, kwa mujibu wa takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Also Read
Mwaniaji urais wa Congo-Brazzaville afariki kutokana na Covid-19

Macron sasa yupo miongoni mwa viongozi watajika ulimwenguni waliopatikana na virusi hivyo, akiwemo Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson.

  

Latest posts

Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdock wakamatwa na kupelekwa mafichoni

Dismas Otuke

Vikosi vya usalama vyazima jaribio la mapinduzi nchini Sudan

Tom Mathinji

China yaadhimisha miaka 50 tangu kurudishiwa kiti chake kwenye Umoja wa Mataifa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi