Rais wa zamani wa FKL Mohammed Hatimy afariki

Aliyekuwa Rais wa shirikisho la kandanda nchini Football Kenya Limited  Mohammed Hatimy  ameaga dunia mapema leo katika Hospitali ya Mombasa kutoka na ugonjwa wa Covid 19 .

Hatimy alikuwa amelazwa katika Hospitali hiyo katika kitengo cha wagonjwa mahututi kwa wiki moja iliyopita na alihudumu kama Rais wa FKL baina ya mwaka 2005 hadi  2011.

Also Read
'Tunatafuta ushindi dhidi ya Comoros na jingine' asema kocha Mulee

Rais wa FKF Nick Mwendwa ameongoza jamii ya soka nchini kuomboleza kifo cha Hatimy akimtaja kuwa kiongozi aliyejituma na kujitolea kwa kazi yake .

Also Read
Harambee Stars yapokea kichocheo cha shilingi milioni 1 kutoka kwa naibu Rais William Ruto

Rais mstaafu wa FKF Sam Nyamweya pia amemwomboleza marehemu waliyefanya kazi kwa pamoja kwa muda mrefu kabla ya kumkabidhi uongozi mwaka 2011 aliposhinda uchaguzi.

Also Read
Misri yafuzu kwenda AFCON 2022 licha ya sare ya 1-1 na Kenya

Baada ya kuondoka katika soka ,Hatimy pia amehudumu  kama mwakilishi wa kaunti mteule  katika bunge la Mombasa na alikuwa mwenyekiti wa kamati ya fedha ya chama cha ODM kaunti ya Mombasa.

 

  

Latest posts

Emmanuel Korir avunja nuksi na kushinda dhahabu ya kwanza ya Kenya Olimpiki mita 800

Dismas Otuke

Chemutai wa Uganda awaduwaza Wakenya na kunyakua dhahabu ya kwanza ya Olimpiki mita 3000 kuruka viunzi na maji

Dismas Otuke

Sydney McLaughlin avunja rekodi ya dunia ya mita 400 kuruka viunzi wanawake katika Olimpiki

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi