Raslimali zaidi zafaa kutengwa kukabiliana na HIV

Mama taifa Margaret Kenyatta amesema ipo haja kuongeza uhamasisho na kutenga raslimali zaidi kwa mipango ya kuzuia na kutibu virusi vya HIV hasa hasa miongoni mwa vijana.

Mama taifa pia anataka kuwe na juhudi zaidi kuwalinda watu walioambukiwza Ukimwi dhidi ya unyanyapaa na kutengwa katika jamii.

Also Read
Sehemu za ibada zatahadharishwa dhidi ya kukiuka sheria za kudhibiti Covid-19

Kwenye ujumbe wake wa kuadhimisha siku ya kukabiliana na janga la Ukimwi duniani, mama taifa amesema amejitolea kukomesha maambukizi mapya ya Ukimwi na msambao wa virusi vya HIV kutoka kwa mama hadi mtoto.

Also Read
Kituo cha kuwatenga wagonjwa wa Covid-19 cha vitanda 29 kujengwa kaunti ya Mandera

Ni kutokana na hayo ambapo Mama taifa alitoa wito kwa kina mama wajawaziti kwenda angalau mara nne kwa kliniki ili kupimwa bila malipo.

Alitoa wito kwa kina mama walio na virusi hivyo kuendelea kwenda kliniki baada ya kujifungua na kutumia dawa za kupunguza makali ya ukimwi jinsi wanavyoagizwa.

Also Read
Kang’ata adai barua aliyomuandikia Rais ilikuwa na nia njema kabisa

Kupitia kwa mpango wake wa Beyond Zero, mama taifa aliahidi kuunga mkono juhudi za serikali za kutimiza lengo la dunia la kuangamiza virusi vya HIV.

  

Latest posts

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi