Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Raymond Shaban Mwakyusa mmiliki wa kampuni ya kusimamia wanamuziki ya Next Level Music – NLM maarufu kama Rayvanny anajipanga Kumtambulisha rasmi msanii wake wa kwanza.

Rayvanny ambaye pia ni mwanamuziki anayesimamiwa na kampuni ya Wasafi WCB tangu mwaka 2015, alifungua rasmi kampuni na studio zake za Next Level Music mwezi Machi mwaka huu wa 2021.

Also Read
Cardi B na Megan Thee Stallion kutumbuiza kwenye Grammys

Wakati huo, alifafanua kwamba angesalia chini ya usimamizi wa kampuni ya WCB kulingana na mkataba wake. Tangu wakati huo kazi ambazo amekuwa akitoa za muziki zina nembo mbili, ya WCB na ya NLM.

Diamond Platnumz anayemiliki WCB alionekana kumuunga mkono akisema ni hatua nzuri aliyochukua ili talanta nyingine nyingi zikuzwe.

Also Read
Mbosso atoa albamu

NLM ilichukua muda kutangaza wasajiliwa wake na alipoulizwa kwenye mahojiano kuhusu kutambulisha wasanii wa NLM, Rayvanny alisema kwamba hakutaka kuharakisha kutambulisha mwanamuziki ambaye hakuwa tayari kwa umma.

Rayvanny tayari amefichua jina na sura ya msanii huyo kifungua mimba wa NLM. Anaitwa Macvoice na atatambulishwa rasmi Ijumaa tarehe 24 mwezi huu wa Septemba mwaka 2021.

Also Read
Lava Lava kuzindua nyimbo zake Kesho
Macvoice

Haya yanajiri siku chache tu baada ya Rayvanny kupiga hatua nyingine maishani ambapo alifungua mkahawa uitwao “Havanna”. Uko katika jumba la kibiashara la Classical, Mbezi Beach.

  

Latest posts

Ogopa Wasanii, Kibao Kipya Cha Willy Paul

Marion Bosire

Kipindi Cha Wendy Williams Kuendelezwa na Watangazaji Tofauti

Marion Bosire

“Upendo” Kibao Kipya Kutoka Kwa Zuchu Na Spice Diana

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi