Ringtone afika mahakamani akiwa kwenye Ambulensi

Mwanamuziki wa nyimbo za injili humu nchini Alex Apoko maarufu kama Ringtone amefika mahakamani akiwa kwenye Ambulensi kwa ajili ya kesi ya kushambuliwa na mwanablogu Robert Alai barabarani siku tano zilizopita.

Kilichosababisha ugomvi huo wa barabarani hakijajulikana lakini kulingana na video zilizosambaa Alai alionekana akiwa amebeba rungu huku akimzomea Ringtone ambaye alikuwa anavuja damu kwenye shavu.

Also Read
Weezdom asihi wakenya wasimchangie Dar Mjomba

Akizungumza na wanahabari, mwimbaji huyo alisema haja yake kubwa sio kulipwa maanake Alai amekuwa akimtumia watu akitaka kumlipa ili aondoe kesi kortini. Kulingana naye, anataka kesi hiyo na adhabu atakayopatiwa Alai iwe funzo kwa wengine ambao wana tabia ya kushambulia watu ovyo.

Ringtone anadai amekuwa na maumivu tangu ashambuliwe kiasi cha kulazwa hospitalini jambo ambalo linalemaza kazi yake ya kila siku ambayo ameitaja kuwa biashara.

Also Read
Rihanna kutoa kibao kipya karibuni!

Asubuhi ya leo, Ringtone aichapisha picha akiwa amelazwa kwenye machela ndani ya Ambulensi akitangaza kwamba kesi kati yake na Alai ingesikilizwa leo saa tatu asubuhi katika mahakama ya Kibera.

Awali alikuwa amechapisha video akiwa ndani ya gari yake akilia na kudai kwamba alikuwa na maumivu makali kwenye kichwa akisema ikiwa ataiaga dunia na ifahamike kwamba Alai ndiye msababishi.

Ringtone huwa mara nyingi anatumia sarakasi za kutunga kama njia ya kusukuma kazi yake ya muziki na hata kisa cha kushambuliwa barabarani na Alai kwa rungu kilipotokea wengi walishindwa kuamini.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi