Kocha wa Tusker Fc Robert Matano ,Zedekiah Zico Otieno wa Kenya Commercial Bank ,Andre Casa Mbungo wa Bandari FC ,Patrick Auseems wa AFC Leopards,William Muluya wa Kariobangi Sharks na Frank Ouna wa Mathare United wameteuliwa kuwania tuzo ya kocha bora wa msimu uliopita wa ligi kuu ya Kenya FKF.
Matano aliongoza Tusker kushinda taji ya ligi kuu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2016 na ya 12 kwa jumla msimu uliomalizika ,huku pia Zico akiwaongoza KCB kuchukua nafasi ya pili ligini kwa mara ya kwanza .
Mshindi wa tuzo hiyo atabainika kwenye hafla itakayoandaliwa Septemba 14