Ronaldo kuachiliwa kuondoka Old Traford

Klabu ya Manchester United imesema iko tayari kumwachilia mshambulizi Christiano Ronaldo ahame msimu huu wa uhamisho.

Ronaldo amesalia na mwaka mmoja kwenye mkataba wake aliosaini tangu atue Old Traford akitokea Juventus mwaka mmoja uliopita .

Also Read
EPL:Msimu mpya wa ligi kuu Uingereza kuwa na mapumziko ya zaidi ya wiki 6 kuruhusu kipute cha la dunia nchini Qatar

Man United wameanza msimu wakitepetea ,wakishindwa mechi mbili mtawalia dhidi ya Brighton na Brentford.

Also Read
Gor Mahia watajilaumu kwa kushindwa kufuzu hatua ya makundi

United wanaburura mkia kwenye jedwali la ligi kuu Uingereza bila ushindi huku wakipangiwa kumenyana na Liverpool Agosti 22.

Also Read
El Bakkali ashinda dhahabu ya mita 3000 kuruka viunzi na kuzima ubabe wa Kenya tangu mwaka 1968

Ronaldo aliye na umri wa miaka 37,ana hadi Septemba mosi kutafuta klabu atakayohamia ,kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho.

  

Latest posts

Msimu mpya wa ligi kuu ya FKF waahirishwa kutoka Oktoba Mosi

Dismas Otuke

KBC Channel One na Idhaa 13 kupeperusha mechi za kipute cha kombe la dunia

Dismas Otuke

FIVB:Kenya yatimuliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha Italia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi