Rudisha atoa hamasa kwa vijana wa Kenya kujituma na kuhifadhi taji

Bingwa wa Olimpiki mara 2 katika mita 800  David Rudisha amewapa hamasa wanariadha wa  Kenya kujituma  wakati wa mashindano ya dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20  yatakayoanza Jumatano na kukamilika tarehe 22 mwezi huu.

Akizungumza kwenye mahojiano ya kipekee na KBC Rudisha ambaye pia ni balozi wa mashindano hayo ametoa changamoto kwa wanariadha wote kutumia  fursa ya kushindanan nyumbani na kutamba.

Also Read
Kenya yang'atwa na Burundi 4-2 na kubanduliwa nje ya CECAFA

“Mashindano haya ndio mwanzo wa kila mwanariadha nakumbuka ndio mashindano yangu ya kwanza nilishinda China mwaka 2006 na kuandaliwa humu nchini ni fursa nzuri kwa chipukizi wetu kung’aa”akasema

“kuwa balozi wa mashindano haya inamaanisha mengi kwangu  na pia nawapa changamoto chipukizi wetu kujituma na kupata ushindi nyumbani,serikali na chama cha riadha Kenya wanapaswa kuekeza zaidi katika mashindano ya ndani ya uwanja ili Kenya isiwe inategemea mbio  pekee”

Also Read
Leopards kukabana koo Rangers wakati Ulinzi wakipambana na Sofapaka Betway Cup

Wakati uo huo Rudisha ambaye pia anashikilia rekodi ya dunia ya mita 800  amesema amepona jeraha na anatarajiwa kutangaza hatma yake hivi karibuni huku akiridhishwa na jinsi Wakenya wamedhihirisha umari wao katika Olimpiki ambapo Kenya haijapoteza dhahabu tangu mwaka 2008.

Also Read
Faith Kipyegon ateuliwa kuwania tuzo ya mwanariadha bora wa mwaka huu

Kenya itakuwa ikitetea taji ya chipukizi waliyonyakua mwaka 2018 mjini Tampere Finland kwa dhahabu 6 fedha 4 na shab 1.

 

  

Latest posts

Bayern Munich wapokea kichapo cha kihistoria 5-0 dhidi ya Borusia Monchengladbach na kutemwa nje ya kombe la DFB

Dismas Otuke

Ronald Koeman atimuliwa Barcelona baada ya kushindwa na Vallecano

Dismas Otuke

Droo ya Safari Sevens yatangazwa Mabingwa watetezi Morans wakikutanishwa na Uhispania

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi