Ruth Chepng’etich ana imani ya Kenya kushinda medali zote za marathon Olimpiki

Bingwa wa dunia wa mbio za marathon Ruth Chepng’etich ana imani kuwa wanariadha wa Kenya watanyakua nishani zote tatu za Olimpiki mwaka huu kwa mara ya kwanza katika historia ya marathon ya wanawake.

Ruth Chepngetich akishiriki mbio za nyika mwezi uliopita

Chepng’etich ambaye maajuzi aliweka rekodi mpya ya dunia ya nusu marathon amesema kikosi cha timu ya Kenya ni dhabiti na kuna uwezo wa histoaria kuandikwa upya mjini Tokyo Japan.

“Mwaka huu kuna uwekezakano wa wakenya kupata medals zote katika marathon ya wanawake ,ukiangalia kikosi tulicho nacho kila mtu yuko katika ubora wake,Brigid ako sawa,Vivian pia ni mzuri na Peres amejipanga vizuri,mimi baada ya kuvunja rekodi ya dunia ya half marathon sasa nalenga niwe kwenye podium wakati wa Olympics “akasema Chepng’etich

Also Read
Jebitok,Kipyegon na Chebet wafuzu kwa nusu fainali ya mita 1500

Kenya haijawaishinda dhahabu ya olimpiki ya marathon kwa wanawake  baada ya Jemima Sumgong aliyekuwa amenyakua dhahabu mwaka 2016 kupigwa marufuku baada ya kupatikana kuwa mlaji muku.

Also Read
Kipkeino classic matayarisho yakamilika

Akizungumza na KBC radio taifa¬† Cheng’etich ameongeza kuwa kuvunja rekodi ya dunia ya half marathon maajuzi mjini Istanbul inampa motisha ya hali ya juu anapoelekea Olimpiki .

“Hiyo world record ni big motivation kwangu ninapojiandaa kwa olimpiki na ilikuja bila kutarajia kwani mimi nilikuwa tu natafuta ushindi lakini tukiwa katikati ya shindano pace maker wangu akaniambia tuko within the world record”akaongeza Chepng’etich

Chepng’etich aliye na umri wa miaka 26 aliandikisha rekodi mpya ya dunia ya nusu marathon aliposhinda mbio za Istanbul half marathon kwa mara ya tatu kwa kuweka muda wa saa 1 dakika 4 na sekunde 2 ,akivunjilia mbali rekodi ya Mhabeshi Ababel Yeshane mwaka 2020 ya saa 1 dakika 4 na sekunde 31.

Also Read
Michezo kufunguliwa tena nchini baada ya kufungwa kwa mwezi mmoja

Mwanariadha huyo kwa sasa ameendelea na mazoezi yake mjini Ngong anapojiandaa kwa michezo ya Olimpiki atakapokuwa akishiriki kwa mara ya kwanza .

  

Latest posts

Omanyala aweka rekodi mpya ya Afrika ya mita 100 ya sekunde 9 nukta 77 Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Wakenya walenga kulipiza cha Olimpiki katika mita 3000 kuruka viunzi na maji katika Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Faith Kipyegon kufunga msimu nyumbani Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi