Ruto akutana na mgombea huru wa uchaguzi mdogo wa Msambweni, Feisal Bader

Naibu Rais William Ruto ameonyesha ishara ya kumuunga mkono mgombea huru wa kiti cha Ubunge cha Msambweni Feisal Abdallah Bader katika uchaguzi mdogo ujao.

Haya yanajiri siku moja baada ya chama cha Jubilee kutangaza kutoweka mgombea katika uchaguzi huo.

Ruto amekutana na Feisal akiwa ameandamana na wabunge Athman Sharif wa Lamu Mashariki, Mohammed Ali wa Nyali, Owen Baya wa Kilifi Kaskazini, Khatib Mwashetani wa Lunga Lunga na Aisha Jumwa wa Malindi.

Also Read
Vyombo vya habari vyaonywa dhidi ya kueneza semi za chuki

Hatua hii inatarajiwa kuamsha upinzani mkali kati ya Ruto na Kinara wa ODM Raila Odinga, ambaye anatarajiwa kuweka mgombea atakayepigania kumrithi mwendazake aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Suleiman Dori ambaye pia alikuwa wa ODM.

Jumatano, Ruto alionekana kumuunga mkono Mariam Sharlet ambaye alikihama chama cha ODM na kujiunga na Jubilee kabla Katibu Mkuu wa chama hicho kutangaza uamuzi wa kutoweka mgombea.

Also Read
Sharlet Mariam ajitoa kwenye uchaguzi mdogo wa Msambweni

Baada ya mkutano na Feisal, Ruto ameandamana na zaidi ya wabunge 40 na kuelekea hadi Kaunti ya Kajiado alikojiunga na jamii ya Matapato katika sherehe ya Olngesher Lool Ilmerishie.

Amewarai viongozi waungane na kukabiliana na changamoto zinazoikumba nchi hii.

Also Read
Wakazi wa Narok wahimizwa kuchukua vitambulisho vyao kwenye Kituo cha Huduma

“Badala ya kutaka kuongeza nafasi serikalini kwa ajili yetu wenyewe, tunapaswa kuzingatia maendeleo ya wananchi. Huu si wakati wa kuwatia Wakenya hofu bali ni wakati wa kuwapa tumaini,” amesema.

Amesema siasa za ukabila na ubabe zimepitwa na wakati na kwamba Wakenya sasa watachagua viongozi kulingana na sifa zao.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi