Ruto alaumu ODM kwa kuhujumu ajenda ya Jubilee

Naibu Rais Dkt. William Ruto amesema  chama cha ODM hakiwezi kujitenga na   hali ya utendakazi duni iliyosababishia serikali ya Jubilee.

Ruto amesema upinzani umekuwa ukihusika katika shughuli za serikali katika muda wa miaka mitatu iliyopita kupitia salamu za maridhiano.

Akiongea katika makazi yake mtaani Karen jijini Nairobi ambapo aliandaa mazungumzo na wawakilishi wa wadi kutoka kaunti ya Mandera wakiongozwa na kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti hiyo  Abdi Adan Ali, naibu rais alisema upinzani ukiongozwa Raila Odinga utawajibika kwa kuchangia  utendakazi duni wa serikali.

Also Read
Nchi zilizostawi zatakiwa kufadhili elimu katika mataifa maskini

“Mnapaswa kulaumiwa kwa kuhujumu ajenda ya maendeleo ya chama cha Jubilee. Hamwezi kuwashutumu wengine,” alifoka naibu rais.

Wakati huo huo naibu rais aliwataka wanasiasa kutoharamisha mashauriano kuhusu mahitaji na maazimio ya wakenya wa kawaida.

Also Read
Raphael Tuju amfokea Naibu Rais William Ruto

Alisema muda umewadia wa mjadala wa kitaifa unaoangazia suala la kuwapa uwezo watu wa viwango vya chini vya maisha.

Dkt. Ruto alisema mashauriano ya kuwapa uwezo watu wa tabaka ya chini hayana lengo la kugawanya wakenya bali kushughulikia matatizo ya wakenya maskini.

“Mazungumzo tuliyonayo si kuhusu matajiri na masikini, ni kuwajumuisha wote katika meza ya mazungumzo na kuhakikisha masalahi ya kila mmoja yanashughulikiwa,” alisema naibu rais

Also Read
NMS kufanyia majaribio kituo cha mabasi cha Green Park Ijumaa jioni

Naibu rais amesema kwa muda mrefu majadiliano ya kitaifa yamekuwa yakihusu viongozi na nyadhifa za uongozi huku mahitaji ya wakenya wa kawaida yakipuuzwa.

Aliwahakikishia viongozi wa Kaunti ya Mandera usaidizi wa serikali katika kukabiliana na changamoto zinazowakumba.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi