Ruto ataka waanzilishi wa ghasia za Murang’a wachukuliwe hatua

Naibu Rais William Ruto ameitaka Idara ya Polisi iwachukulie hatua wale waliohusika katika kupanga ghasia zilizoshuhudiwa huko Murang’a Jumapilizilizopelekea watu wawili kuaga dunia.

Ruto amesema wahusika hao wanajulikana vizuri na wanapaswa kuadhibiwa bila kuzingatia misimamo yao ya kisiasa.

“Vyombo vya usalama vinawajua wale walioanzisha hizo ghasia. Lazima wachukuliwe hatua bila kujali msimamo wao wa kisiasa,” amesema.

Also Read
Wakazi wa Narok waonywa dhidi ya kulegeza kanuni za COVID-19

Amesema ghasia hizo za Murang’a zilikuwa ni mwendelezo wa yale yaliyotukia Kaunti ya Kisii mwezi uliopita ambapo kundi la vijana lilipelekwa eneo hilo kuzusha vurugu wakati wa ziara yake ya kimaendeleo.

“Hii ilitukia Kajiado pia siku chache zilizopita ambako utawala wa eneo hilo ulitumika kutishia wananchi ili wasihudhurie hafla yangu,” akasema.

Also Read
Huenda wasichana wengi wasirejee shuleni kutokana na mimba za mapema

Ruto amesema haya nyumbani kwake Karen kwenye mkutano na zaidi ya viongozi 2,000 wa nyanjani kutoka Kaunti ya Narok.

Amesema licha ya vitisho hivyo, hatasita kutekeleza wito wa kuwainua wananchi kupitia miradi mbali mbali na akaahidi kuongeza juhudi zaidi.

Also Read
Mpango wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu ustawi wa kiviwanda wazinduliwa

“Najua ni vigumu lakini lazima tuwe na mjadala huu. Tutazidisha juhudi hizi ili kuwezesha kila mmoja,” akahoji.

Ruto amesikitishwa na madai kuwa polisi wanazidi kutumika kutekeleza maswala ya kisiasa na akamsihi Inspekta Jenerali wa Polisi asalie upande wa haki na kuwahudumia Wakenya wote sawa sawa bila ubaguzi.

  

Latest posts

Nabulindo ashinda kesi ya kupinga kuchaguliwa kuwa mbunge wa Matungu

Dismas Otuke

Kenya yanakili visa vilivyopungua zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Ibada ya wafu ya daktari Gakara na wanawe wawili yaandaliwa Nakuru

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi