Ruto awataka wakazi wa Pwani kugura ODM na kuunga mkono UDA

Naibu wa Rais Dkt. William Ruto ametoa wito kwa wakazi wa eneo la Pwani kuunga mkono azma yake ya kuwa Rais wa nchi hii wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Naibu huyo wa Rais aliwapa changamoto wakazi hao kukigura chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga na kujiunga na chama cha UDA ili kumwezesha kubuni serikali ijayo.

Also Read
Taharuki yatanda Mandera kufuatia mauaji ya mchungaji mmoja wa mifugo

“Nawahimiza msicheze shere tena na siku zenu zijazo,” Ruto aliyasema hayo katika kaunti ya Kilifi wakati wa mazishi ya kasisi George Mwangome Chipa na ndugu yake Adam Goe Chipa.

Ruto alidai kuwa  Raila hana rekodi ya maendeleo na hapaswi kuaminiwa kwa uongozi.

“Ikiwa mtu hana historia ya kujenga barabara, kuwaunganishia wananchi nguvu za umeme, kutengeneza taasisi za kiufundi au kununulia shule basi, ni miujiza ipi ataifanya kufufua uchumi,”  aliuliza Ruto.

Also Read
Maelfu ya Wakenya wapoteza ajira kutokana na janga la COVID-19

Kulingana na Ruto, yeye ndiye bora zaidi kuboresha uchumi wa wakazi wa Pwani huku akiwataka viongozi kuzingatia maendeleo yatakayoboresha maisha ya wakazi. Dkt.  Ruto alisema kuwa wakenya wanataka siasa zitakazoleta maendeleo.

Also Read
Ajuza wa miaka 70 auawa Nyamira kwa madai ya kumroga mjukuu wake

“Walio na njaa wanataka chakula sio kubadilishwa kwa katiba. Mazungumzo yetu yatahusisha uchumi na kuwawezesha mamilioni ya wakenya wanaoishi na ufukara,” alisema Ruto.”

Naibu wa Rais alikuwa ameandamana na mbunge wa Kilifi Kusini Richard Chonga mwenzake wa Kaloleni  Paul Katana, Benjamin Tayari  wa Kinango,  Owen Baya wa  Kilifi North kaskazini na  Aisha Jumwa wa Malindi.

  

Latest posts

Vifo vya ndugu wawili vyazua taharuki Embu Kaskazini

Tom Mathinji

Gladys Erude ameaga dunia

Marion Bosire

Cheruiyot, Simotwo na Kipsang kushiriki nusu fainali ya mita 1500

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi