Ruto azuiwa kutumia Afisi za Makao Makuu ya Jubilee

Naibu Rais William Ruto sasa hataruhusiwa kutumia afisi za Makao Makuu ya Chama cha Jubilee katika mipangilio yake ya kuwania urais kufuatia uamuzi wa Kamati ya Kitaifa ya chama hicho.

Kamati hiyo pia imependekeza kuondolewa kwa Ruto kutoka nafasi ya Naibu Kinara wa chama cha Jubilee wakihoji kuwa ameunda chama chengine cha Jubilee Asili anachonuia kukitumia katika uchaguzi mkuu wa 2022.

Also Read
Ghasia zashuhudiwa katika mkutano wa Ruto huko Murang’a

Katibu Mkuu wa Jubilee Raphael Tuju amesema uamuzi wa Ruto kuzuru Makao Makuu ya Jubilee hapo jana akiandamana na baadhi ya wabunge haukuwa wa sawa na ulinuia kumkejeli Rais Uhuru Kenyatta.

Also Read
COVID-19: Watu 302 zaidi waambukizwa huku wagonjwa 17 wakifariki

Tuju amesema wabunge hao walioandamana na Ruto ni wale wanaomtusi Rais Kenyatta kila mara na akaongeza kuwa chama hicho kililazimika kuingilia kati ili kuzuia uwezekano wa mafarakano na wabunge wanaoegemea upande wa Rais waliotishia kuelekea katika makao makuu hayo pia.

Also Read
Viongozi wa Jubilee eneo la Mlima Kenya wataka kubadilishwa kwa uongozi wa

Aidha,Tuju amesema Ruto hataruhusiwa kutumia Makao Makuu ya Jubilee kwa kujitafutia umaarufu katika azma yake ya kuwania urais mwaka wa 2022.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi