Ruto: Orodha ya mali yangu iliyowasilishwa bungeni ni ya kupotosha

Naibu Rais Dkt. William Ruto amepuuzilia mbali kikao cha kamati ya bunge kuhusu utawala na usalama wa kitaifa akitaja kikao hicho kuwa njama za kusuluhisha tofauti za kisiasa kwa kutumia takwimu za uwongo.

Alisema wizara ya usalama wa kitaifa, ilipanga kujiwasiliswa kwake bungeni kwa lengo la kutaka kukagua mtindo wake wa maisha.

Alikanusha kwamba yeye ndiye mmiliki wa baadhi ya mali zilizoorodheshwa na waziri wa usalama wa kitaifa Dkt. Fred Matiang’i.

Also Read
Mwanasiasa Mashuhuri Simeon Nyachae kuzikwa tarehe 15 mwezi Februari

Ruto alisema hatua hiyo iwapo ni ya halali, inapaswa kuwashirikisha viongozi wote.

Huku akitaja kikao cha kamati hiyo kuwa kisicho na maana, Naibu Rais alisema habari kuhusu idadi ya maafisa wanaomlinda ni ya kupotosha.

Alisema baadhi ya viongozi wanajishughulisha na mambo yasiyo na maana badala ya kushughulikia matatizo halisi yanayokabili ma-milioni ya wakenya wa kawaida.

Also Read
Nairobi yaongoza kwa Idadi ya vijana waliojisajili kwa kazi Mtaani

Baadhi ya mali yaliyoorodheshwa kumilikiwa na naibu Rais ni pamoja na Kitengela Gas, Weston Hotel, shamba la Murumbi huko (Narok), shamba la ufugaji la ADC huko Laikipia, Hoteli ya Dolphine huko Mombasa, shamba la Mata huko Taita Taveta, Elgon View huko Eldoret, shamba la ufugaji Kuku la Koitalel na pia makaazi ya kibinafsi ya Kosachei.

Naibu huyo wa Rais alizungumza Alhamisi wakati wa mkutano na viongozi wa mashinani kutoka maeneo bunge ya Bahati, Subukia, Nakuru Mashariki, Nakuru Magharibi, Molo na  Rongai katika makazi yake ya Karen Jijini Nairobi.

Also Read
William Ruto: Nitakubali matokea ya Uchaguzi Mkuu

Susan Kihika, David Gikaria, Irungu Kang’ata, Mathias Robi, Kimani Ichung’wa, Gathoni Wa Muchomba, Rahab Mukami, Wangui Ngirici, Cecily Mbarire, Nimrod Mbai, Kimani Ichung’wah, Millicent Omanga, Kipchumba Murkomen, Silvanus Osoro na Rigathi Gachagua walikuwa miongoni mwa wabunge waliohudhuria mkutano huo.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi