Ruto: Nitawahudumia Wakenya wote kwa usawa

Kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa Rais mteule wa Jamuhuri ya Kenya, naibu Rais Dkt. William Ruto aliandaa mkutano na viongozi wa muungano wa Kenya Kwanza waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu uliopita.

Katika mkutano huo ambao ulilenga kutoa mwongozo na kujiandaa kwa majukumu ya serikali ijayo, Ruto alisema kuwa atashirikiana na wakenya wote katika kutekeleza ahadi zake kwa taifa hili.

Aidha Rais huyo mteule, alihakikisha kuwa, hakuna afisa yeyote wa serikali ambaye atahujumiwa, huku akiwataka watumishi wa umma kuwahudumia wakenya ipasavyo..”Tutawahudumia wakenya wote.

Also Read
Ruto asema ataboresha uchumi wa Pwani akichaguliwa Rais
Also Read
Rais Kenyatta amwomboleza spika wa zamani wa kaunti ya Nairobi Alex Magelo

“Tutajizatiti kutimiza ahadi zetu kwa wakenya. Tutawahudumia wote kwa usawa. Hii itakuwa serikali yenu, serikali ya watu wa Kenya,” alisema Dkt.Ruto.

Viongozi waliochaguliwa chini ya muungano wa Kenya Kwanza wakutana na Rais Mteule William Ruto.

Rais huyo mteule alidokeza kuwa mawaziri katika serikali yake kamwe hawatakosa kuhojiwa na kamati za bunge, kwa kuwa serikali yake inapigania uwazi na uwajibikazi.

Also Read
Asilimia 90 ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wafika shuleni

Alionya kuwa mawaziri katika serikali yake hatakubaliwa kushiriki katika maswala ya kisiasa, lakini watalenga kuwahudumia wakenya.

“Ushindi wetu katika Uchaguzi Mkuu uliopita ni kutokana na nguvu za Mungu,”

  

Latest posts

Wetangula kuamua Alhamisi ni chama kipi kitashikilia wadhifa wa kiongozi wa wengi bungeni

Tom Mathinji

Gavana Orengo awatuma maafisa wakuu wa kaunti kwa likizo ya lazima

Tom Mathinji

Kipchoge na Kipruto warejea nyumbani kutoka London

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi