Majirani Uganda Cranes na Amavubi ya Rwanda walitoka sare tasa katika mechi ya pili ya kundi C ya kombe la CHAN iliyopigwa Jumatatu usiku katika uwanja wa Reunification mjini Doula Cameroon.
Timu zote mbili zili zilikuwa na nafasi nyingi za kufunga mabao huku makipa wakilazamika kufanya kazi ya ziada ambapo mikwaju ya wachezaji Jaques Tuyisenge ,Betrand Iradikunda na Ange Musinzi ikipanguliwa na kipa wa Uganda Patrick Lukwago na mabeki wa Uganda katika kipindi cha kwanza.
Upande wa pili wa sarafu matobwe ya Waganda walipoteza nafasi za wazi kipindi cha kwanza huku mikwaju ya Milton Karisa ,Bright Akukani na Brian Aheebwa ikipanguliwa kipindi cha kwanza .
Kipindi cha pili timu zote zilicheza kwa tahadharri kuu na hadi kipenga cha mwisho Derby hiyo ya Afrika Mashariki ikamalizika kwa sare ya bila bila.
Awali Moroko walisajili ushindi wa bao 1 -0 dhidi ya Togo ,bao la dakika ya 27 kupitia mkwaju wa penati uliofungwa na Yahya Jebrane.
Moroko ambao ni mabingwa watetezi wanaongoza kundi hilo kwa alama 3 wakifuatwa na Uganda na Rwanda kwa alama 1 kila moja wakati Togo ikiburura mkia bila alama.