Safari ya Afrika kwenda kombe la dunia Qatar mwaka ujao yaahirishwa hadi Oktoba

Shirikisho la kandanda Afrika Caf limetangaza kuahirisha  mechi za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao nchini Qatar kutoka mwezi Juni hadi  Oktoba.

Caf imesema kuwa imebidi kuahirisha mechi hizo kutokana na changamoto zilizoletwa  na janga la Covid 19 .

Also Read
FIBA Afrobasket yaingia kwota fainali Jumatano Kigali

Kulingana na kamati kuu ya CAF  mechi hizo sasa zitaanza Oktoba na kumalizika Machi mwaka 2022.

Habari hizo ni afueni kwa timu nyingi ambazo zilikuwa hazijajiandaa vyema haswa baada ya kukamilisha mechi za kufuzu kwa kombe la AFCON mwezi Machi mwaka huu.

Also Read
Sudan kipiga kambi ya mazoezi Dubai kujiandaa kwa mechi za kufuzu kombe la dunia

Harambee stars imejumuishwa kundi E la safari ya kwenda Qatar pamoja na The Flying Eagles ya Mali,Uganda Cranes na Amavubi ya Rwanda na waatanza harakati za kufuzu dhidi ya Uganda Cranes jijini Nairobi kabla ya kuzuru Kigali dhidi ya Rwanda.

Also Read
Kipyegon na Chepkoech kupiga matayarisho ya mwisho Monaco Diamond league Ijumaa usiku

Timu bora kutoka kila kundi itafuzu kwa raundi ya pili na ya mwisho ambapo washindi watano watawakilisha Afrika katika fainali za kombe la dunia kati ya Novemba 21 na Disemba 18 nchini Qatar mwaka ujao.

 

 

  

Latest posts

Malkia Strikers yafunga mechi za makundi kwa kuilaza Burundi seti 3-0 mashindano ya kuwania kombe la Afrika

Dismas Otuke

Waziri wa zamani wa michezo Hassan Wario afungwa miaka 6 gerezani na kulipa faini ya shilingi milioni 3 nukta 6

Dismas Otuke

Bingwa mara tatu wa dunia Justin Gatlin awasili tayari kushiriki Kip Keino Classic Jumamosi

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi