Safari ya Kisiasa ya Martha Karua

Safari ya kisiasa ya Martha Karua iling’oa nanga mwaka 1991 alipowania kiti cha ubunge cha Gichugu, wadhifa alioushikilia hadi mwaka 2013. Baadaye mwaka 2013, Karua aliwania kiti cha Urais na kuambulia patupu baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutwaa wadhifa huo.

Also Read
Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yang'oa nanga Kisii

Karua kisha alijitosa uwanjani kuwania wadhifa wa Ugavana wa Kirinyaga na kubwagwa nje na Gavana wa sasa Anne Waiguru. katika uchaguzi huo Karua alipata kura 122,091 huku Waiguru akizoa kura 161,373.

Hapo awali, Karua alishikilia nyadhifa kadhaa serikali, ambapo mwaka 1981 hadi mwaka 1987, alikuwa hakimu katika mahakama za Makadara, Nakuru na Kibera.

Also Read
Kesi ya Narc Kenya dhidi ya IEBC yatupiliwa mbali

Mnamo mwaka 2003 hadi 2005 karua alichaguliwa kuwa waziri wa maji na unyunyizaji mashamba maji, kabla ya kuhamishwa kwa wizara ya haki na maswala ya katiba, kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2009.

Also Read
Martha Karua: Sina haraka ya kumuunga mkono mwaniaji yeyote wa kiti cha Urais

Mwanasheria huyu wa Gichugu alibuni kampuni ya Martha Karua and Co. Advocates mwaka 1987.

Karua anafahamika sana kwa misimamo yake mikali hasaa katika mijadala ya bunge za kitaifa.

 

  

Latest posts

Shikanda ahifadhi uenyekiti wa AFC Leopards

Dismas Otuke

Kalle Rovanpera atwaa ubingwa wa raundi ya Kenya mashindano ya WRC

Tom Mathinji

Ajali ya kwanza yatokea katika barabara ya Expressway

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi