Safari ya Rais John Pombe Magufuli Ikuluni

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, alizaliwa tarehe 29 mwezi Oktoba mwaka 1959 katika Wilaya ya Chato kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Hapo awali wilaya ya Chato ilikuwa sehemu ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera na ilihamishwa hadi mkoa wa Geita mwaka 2012.

Magufuli alisomea katika shule ya msingi ya Chato  kuanzia mwaka 1967 hadi 1975 kabla ya kujiunga na shule ya sekondari ya awali katika Seminari ya Katoke, Biharamulo.

Kisha kiongozi huyo wa chama cha mapinduzi alimalizia kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Lake, mkoani Mwanza.  Magufuli alimaliza Kidato cha sita akiwa katika shule ya upili ya Mkwawa mkoani Iringa.

John Pombe Magufuli alipata cheti cha Stashahada ya Ualimu kutoka chuo cha Elimu Mkwawa mwaka 1982.

Also Read
Trump abadili mpango wa kutaka maafisa wa White House wawe wa kwanza kupokea chanjo ya COVID-19

Kati ya mwaka 1985 na 1988, Magufuli alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya masomo yake ya shahada ya kwanza ya ualimu wa kemia na hisabati.

Baadaye Magufuli  alifuzu kwa shahada ya uzamili katika somo la kemia katika chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kile cha Salford cha Uingereza mtawalia kati ya mwaka 1991 na 1994.

Rais huyo wa Tanzania alifundisha masomo ya hisabati na kemia katika shule mbalimbali za sekondari nchini Tanzania kuanzia mwaka 1983.

Magufuli ni mwanachama wa chama cha Wakemia wa Tanzania na kile cha Wataalamu wa Hisabati Tanzania.

Kiongozi huyu hajaachwa nyuma katika tasnia ya uandishi, kwani amechapisha nakala kadhaa hasaa kuhusu maswala ya kisayansi. 

Also Read
Mohamed Bazoum atangazwa kuwa Rais mpya wa Niger

Aliingia vipi katika siasa?

Mnamo mwaka 1995, John Magufuli alijiunga katika baraza la Mawaziri kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa kuwa waziri msaidizi katika wizara ya ujenzi.

Uteuzi huo katika baraza la mawaziri ulijiri baada ya kiongozi huyo kuchaguliwa mbunge wa chato mwaka uo huo.

Alipanda ngazi na kushikilia wadhifa wa uwaziri katika wizara kadhaa kama vile wizara ya Ujenzi, ile ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi sawia na wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Magufuli alijitosa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa urais kilichoandaliwa tarehe 25 mwezi Oktoba mwaka 2015 ambapo alimshinda mpinzani wake mkuu Edward Lowassa wa chama cha Chadema.

John Pombe Magufuli aliapishwa tarehe 5 Mwezi Novemba kuwa Rais wa tano wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Also Read
Ugiriki yalegeza masharti ya kudhibiti Covid-19 kuwavutia watalii

Huku muhula wa kwanza wa miaka mitano wa rais John Magufuli ukifika ukingoni, chama tawala cha CCM kimemteua kuwania muhula wa pili wa mwaka 2020 hadi 2025.

Awamu hiyo ya kwanza ya Magufuli madarakani imekosolewa na wadadisi hasaa katika uhusiano wa Tanzania na mataifa ya kigeni. Uhuru wa uandishi wa habari pia umetajwa kuzorota nchini humo.

Hata hivyo muhula huo wa kwanza wa Magufuli umesifiwa kwa kuleta mabadiliko makubwa nchini humo hasaa katika miundo msingi, uchukuzi hasaa wa baharini.

Ukakamavu wa Magufuli pia umesifiwa kwa kuangamiza ufisadi nchini Humo.

Mbivu na mbichi itafahamika tarehe 28 mwezi Oktoba wakati uchaguzi mkuu utaandaliwa nchini Tanzania.

  

Latest posts

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika azikwa Jijini Algiers

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Ethiopia yakaribisha wito wa kurejelewa mazungumzo na majirani wake kuhusu bwawa katika mto Nile

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi