Safari za ndege zasitishwa nchini China kutokana na Kimbunga In-Fa

Viwanja viwili ya kimataifa vya ndege kwenye mji wa Shanghai nchini China, vimeahirisha safari zote za ndege huku maafisa wakitoa wito kwa wakazi kusalia manyumbani kwao kwenye eneo hilo la mashariki mwa China ambayo limekumbwa na kimbunga kikubwa cha In-Fa.

Also Read
Msako dhidi ya pombe haramu waanzishwa Nakuru

Kimbunga hicho cha In-Fa kilikumba eneo la Putuo kwenye mji wa Zhoushan,ulioko na bandari kubwa mashariki mwa jimbo la Zhejiang siku ya Jumapili kulingana na shirika rasmi la utangazaji nchini China la CCTV.

Mamia ya safari za ndege katika viwanja vya ndege vya Shanghai Pudong na  Shanghai Hongqiao, zilifutiliwa mbali huku safari zaidi zikitarajiwa kufutiliwa mbali Kulingana na vyombo vya habari vya nchi hiyo.

Also Read
Wasichana tisa waondoka shuleni katika hali tatanishi

Takriban watu 58 wamefariki na wengine zaidi ya milioni moja wakikosa huduma za umeme na kulazimika kuhama.

Also Read
Hatimaye vyombo vya habari vya magharibi vimeanza kuzungumia maabara ya virusi vya Fort Detrick ya Marekani

Siku ya Jumamosi meli kubwa za uchukuzi ziliondolewa kwenye bandari ya Yangshan huko Shanghai kufuatia kimbuga hicho.

Maafisa wa ukoaji watumia matinga tinga na mashua kuwaokoa wakazi waliokumbwa na mafuriko.

  

Latest posts

John Nkengasong: Omicron sio virusi vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Maambukizi ya Covid-19 yazidi kuongezeka Afrika Kusini

Tom Mathinji

Mashabiki 10,000 kuingia Nyayo kwa mechi ya Gor Mahia dhidi ya Otoho Jumapili

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi