Sai Kenya Akana Tetesi Kwamba Ameolewa

Mwanamuziki wa Kenya Grace Sai maarufu kama Sai Kenya ambaye anafanya kazi chini ya Shirko Media, amekana tetesi kwamba alishaolewa kutokana na kimya chake kirefu. Mwanadada huyo ambaye anajiita “The Maasai Empress” amekuwa kimya kwa muda wa mwaka mmoja sasa tangu alipotoa kibao chake kwa jina “Unaboa”.

Akizungumza na Makuu na Ken 1Gb kwenye kipindi Mashav Mashav ndani ya Pwani Fm na runinga ya KBC, Sai alielezea kwamba alinyamaza tu mitandaoni ila studioni amekuwa akijituma kutayarisha kazi nyingine za muziki.

Also Read
Columbus Short kuigiza kama Martin Luther King Jr

Sai alikubali kwamba amebadili dini kutoka Ukristo hadi Uisilamu ambapo alielezea kwamba familia yake nzima ilisilimu akiwa mtoto mdogo, akawa anipenda dini hiyo lakini hakupata mafunzo ya kutosha ndiposa akarejelea Ukristo ila sasa tena amerejelea Uisilamu.

Also Read
Mediocre! Kibao kipya cha Ali Kiba

Kuhusu kiasi cha mahari alisema kwamba yeye anadai milioni kumi kwa yeyote anayetaka kumwoa.

Sai aliwahi kuzuru Tanzania ambapo alitagusana na Babu Tale mmoja wa mameneja wa msanii Diamond Platnumz chini ya Wasafi WCB ambaye aliridhishwa na kazi yake na anatumai kwamba siku moja atashirikiana nao kikazi. Alimtaja pia msanii wa Tanzania Aslay kama mmoja wa wasanii ambao angependa kushirikiana nao katika muziki.

Also Read
Ujio mpya wa Darubini michezo

Kazi ya hivi punde kutoka kwa Sai Kenya ni “Alehandro” ambayo iliachiliwa rasmi tarehe 4 mwezi huu wa Septemba mwaka 2021. Dada huyo ametoa hakikisho kwa mashabiki wake kwamba amerejea kikamilifu na hatachukua mapumziko tena.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi