Samba Boys waanza kwa makeke safari ya kwenda Qatar mwaka 2022

Mabingwa mara tano wa dunia Brazil maarufu kama Samba Boys walianza vyema harakati za kufuzu kwa dimba la mwaka 2022 nchini Qatar baada ya kuwanyofoa Bolivia mabao 5-0 katika mechi iliyopigwa mapema jumamosi  mjini Sao Paulo.

Mshambulizi Roberto Firminho  alifunga mabao 2,huku Marquinhos na  Coutihno wakiongeza moja kila mmoja wakati Bolivia wakajifunga bao jingine.

Also Read
Argentina waweka miadi kukwangurana na Brazil fainali ya Copa Amerika

Brazil inalenga kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 ,likiwa taifa pekee kucheza Makala yote ya kombe la dunia tangu yaanzishwe mwaka 1930 nchini Uruguay.

Also Read
Safari ya kwenda Qatar 2022 yaanzia Amerika Kusini

Mshambulizi Luis Muriel wa Atalanta Fc alipachika kimiani mabao 2  na mwenzake pia wa Atalanta Duvan Zapata akafunga moja ,mabao yote yakifungwa kipindi cha kwanza.

Mechi za mzunguko wa pili hatua hiyo ya makundi kusakatwa kati ya Tarehe 13 na 14 mwezi huu.

Also Read
Ujenzi wa viwanja vya kombe la dunia wakaribia kukamilika

Eneo la Conmebol lina mataifa 10 huku timu  4 bora baada ya mechi zote zikifuzu kwa kipute cha kombe la dunia nchini Qatar kuanzia Novemba mwaka 2022.

 

  

Latest posts

Bayern Munich wapokea kichapo cha kihistoria 5-0 dhidi ya Borusia Monchengladbach na kutemwa nje ya kombe la DFB

Dismas Otuke

Ronald Koeman atimuliwa Barcelona baada ya kushindwa na Vallecano

Dismas Otuke

Droo ya Safari Sevens yatangazwa Mabingwa watetezi Morans wakikutanishwa na Uhispania

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi