Sammy Kasule aaga dunia

Mwanamuziki huyo wa asili ya Uganda aliaga dunia tarehe 27 mwezi Aprili mwaka huu wa 2021 akiwa safarini kuelekea Uswidi kwa ajili ya kupata matibabu zaidi.

Taarifa kuhusu kifo cha mwanamuziki huyo tajika wa Afrika mashariki ambaye aliwahi kuwa kwenye bendi ya Afrigo zilidhititishwa na bendi yake iitwayo “Ziwuuna” kupitia ukurasa wao wa Facebook.

Kulingana na taarifa hiyo, Kasule alionekana kuhitaji usaidizi wa dharura alipofika Amsterdam huko Uholanzi na hapo ndipo alikata roho.

Also Read
Davido aonekana kwenye filamu "Coming 2 America"

Kifo cha Sammy Kasule kimejiri yapata miaka miwili tangu arejee Uganda kutoka Uswidi ambako aliishi kwa miaka 30. Atakumbukwa kwa ufasaha wake katika kucheza gitaa la bass na katika kuandika nyimbo talanta ambazo zilimpa nafasi yake katika ulingo wa muziki aina ya soukous na rumba Afrika Mashariki.

Samuel Kasule, alianza kazi ya muziki katika bendi iitwayo Kawumba mwaka 1969 kabla ya kuhamia nchini Kenya kufuatia mashafuko ya kisiasa nchini Uganda wakati wa uongozi wa Idi Amin.

Also Read
Jeshi la Uganda latoa onyo kali dhidi ya jaribio lolote la mapinduzi

Akiwa Kenya alijiunga na bendi ya Orchestra Les Noirs iliyokuwa na wanachama wa asili ya Congo na baadaye akaingia kwenye bendi ya Liwanza.

Baadaye alitoa kibao chake binafsi kwa jina ‘Mari Wandaka’, ambacho kilipendwa sana nchini Kenya.

Yeye, mcheza gitaa wa aseili ya Congo Tabu Frantal na mcheza kibodi Botango Bedjil waliunda bendi kwa jina Vundumuna ambapo alisalia kwa muda kabla ya kuhamia Uswidi mwaka 1983.

Also Read
Maafisa wa usalama nchini Uganda washtumiwa kwa kuwajeruhi wanahabari waliokuwa wakiripoti kumhusu Bobi Wine

Akiwa huko Uswidi alishirikiana na wanamuziki wengine wa asili ya Afrika katika bendi za Savanna na Makonde.

Vibao ninavyohusishwa na Kasule ni kama vile ‘Ushirikiano’, ‘Kukupenda’, ‘Ndoto’, ‘Ekitobero’ na ‘Shauri Yako’, ambavyo vilisaidia kuendeleza fani yake kama mwanamuziki.

Amewahi kutagusana katika utumbuizaji na wanamuziki kama vile Phillip Lutaaya, Manu Dibango na kundi la Boney M.

  

Latest posts

Waigizaji Wa Nollywood Wazuru Zanzibar kwa Fungate

Marion Bosire

Betty Kyallo Apata Kazi ya Kuigiza

Marion Bosire

Gurdian Angel Asifia Mpenzi Wake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi