Sanaipei Tande akana kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Otile Brown

Mwanamuziki na muigizaji Sanaipei Tande amesema kwamba hajawahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki mwenza Otile Brown.

Akizungumza kwenye mahojiano na Kadzo Mungela katika kipindi cha Kudzacha cha runinga ya KBC, Sanaipei alielezea kwamba yeye ni muigizaji na ikija kazi kama ile ataigiza tu.

Swali hilo likitokana na vibao Chaguo la moyo na Aiyana ambavyo Otile amemshirikisha Sanaipei na kwenye video wanaonekana wakiigiza kama wapenzi.

Also Read
Muigizaji maarufu wa Mombasa Pretty Mutave aaga dunia

Kutokana na hilo Sanaipei alisema kwamba anakerwa sana na wasanii ambao wanatumia vitendo visivyo vya kweli kusukuma kazi zao. Alitoa mfano wa wasanii kudanganya kwamba wana uhusiano wa kimapenzi na sio kweli ili kuendeleza kazi zao.

Msanii huyo mzaliwa wa Mombasa alihimiza wasanii waunde kazi nzuri ambayo hawatahitajika kutumia hila kusukuma.

Also Read
Otile Brown asajili msanii kwenye kampuni yake ya muziki

Kuhusu uigizaji, Sanaipei alisema kwamba hakuwahi kwenda kutafuta hiyo kazi bali alipatiwa nafasi na rafiki yake Eve D’Souza na alipoona anaweza akampa nafasi nyingine kabla ya kipaji chake kuridhisha Rashid Abdalla.

Baadaye Rashid ambaye ni mwandishi, mtayarishi na mwelekezi wa vipindi akampa kipindi Aziza ambapo alikuwa mhusika mkuu. Tangu wakati huo anasema amekuwa tu akipata kazi za uigizaji.

Also Read
Mwanamuziki Bow Wow kuingilia mieleka

Sanaipei Tande alianza muziki kupitia kwa shindano la Coca-cola Popstars la Afrika Mashariki mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 19 tu.

Baadaye yeye na washindi wengine kwenye shindano hilo Pam Waithaka na Kevin Waweru wakaanzisha Kundi la muziki kwa jina “Sema”.

Kundi hilo lilisambaratika muda mfupi baadaye na Sanaipei Tande akaamua kuendeleza muziki wake peke yake hadi sasa.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi