Chama cha riadha Kenya kimeandaa seminaa ya mafunzo dhidi ya ulaji muku siku ya Ijumaa katika mkahawa wa Queens Garden mjini Eldoret.
Seminaa hiyo iligawanywa kwa mafungu matatu ya chipukizi , chipukizi wanaojiung na mashindano ya watu wazima na wanariadha wa kulipwa .
Wanariadha walipokea mafunzo kuhusu ukiukaji wa sheria za ulaji muku na ,madhara ya kutumia dawa za kututumua misuli .
Seminaa hiyo inayoongozwa na maafisa kutoka kutoka shirika la kupambana dhidi ya ulaji muku nchini ADAK , imehudhuriwa na zaidi ya wanariadha 200, watakaoshiriki mashindano ya kitaifa ya mbio za Nyika Jumamosi kijiji cha Lobo mjini Eldoret,kaunti ya Uasin Gishu .
Mashindano ya kitaifa ya mbio za nyika yataandaliwa Jumamosi huku wanariadha kutoka regions zote 16 zilizo chini ya mwavuli wa riadha Kenya waking’ang’ania ubingwa wa kitaifa.

Rais wa chama cha Riadha Kenya Jenerali mstaafu Jackson Tuwei ,aliwahimiza wanariadha kutilia mkazo na kutafuta ufafanuzi kuhusu ulaji muku huku wakidumisha kukimbia bila kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.
“Leo tumemaliza ,lakini hii haimaanishi tutamalizia mazungumzo haya hapa .Tuulize maswali na kutafuta ufafanuzi kuhusu ulaji muku huku tukilenga kuendeleza kampeini ya kuwahamasisha wanariadah kukimbia bila kutumia dawa hizo haramu “akasema Tuwei