Senegal na Burkina Faso kumenyana Jumatano usiku kuwania tiketi ya kucheza fainali ya AFCON

Teranga Lions ya Senegal watashuka katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde Cameroon kwa nusu fainali ya kwanza dhidi ya BUrkina Faso kwenye kipute cha AFCON .

Timu zote mbili zinawinda kombe la AFCON kwa mara ya kwanza lakini mwanzo itabidi wapambane katika derby ya west Africa Jumatano usiku.

Burkinabe ilimaliza katika nafasi ya 3 kwenye makala ya mwisho waliyoshiriki ya mwaka 2017 nchini Gabon na wanajivunia kuamliza nafasi ya pili mwaka 2013 yakiwa matokeo yao bora.

Also Read
Nahodha wa Gabon Pierre Aubemeyang atundika daluga soka ya kimataifa

Timu zote kando na kuwania kombe kwa mara ya kwanza ,pia zinafunzwa na makocha wa nyumbani ,Burkinabe ikiwa na Kamou Malo,nao Senegal wananolewa na nahodha wa zamani ,Aliou Cissé wakimaliza nafasi ya pili mwaka 2019.

Also Read
Mataifa 16 yatakayoshiriki CHAN 2021 kuanzia Jumamosi Januari 16

Senegal watacheza nusu fainali kwa mara ya 5,baada ya kumaliza nafasi ya nne mwaka 1965 na 1990 ,kuchukua nafasi ya pili mwkaa 2002 na nambari nne mwaka 2006 na kuchukua nafasi ya pili tena mwaka 2019.

Simba wa Teranga pia wanajivunia kutopoteza mechi tangu kuanza kwa makala ya mwaka huu.

Also Read
Pitso Mosimane kukutana na waajiri wake wa zamani Mamelodi katika ligi ya mabingwa Afrika

Burkina Faso maarufu kama the Stallions watakuwa wakicheza nusu fainali kwa mara ya nne wakijivunia kumaliza katika nafasi ya nne mwaka 1998,nambari 2 mwaka 2013 na kutwaa nafasi ya tatu mwaka 2017.

Burkinabe wamepoteza mchuano mmoja pekee waliopigwa katika hatua ya makundi na wenyeji Cameroon.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi