Seneta maarufu wa upinzani nchini Cameroon auawa

Seneta mmoja maarufu wa upinzani ambaye pia ni wakili nchini Cameroon ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa Bamenda kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki walimlazimisha seneta Henry Kemende, kutoka ndani la gari lake kabla ya kumpiga risasi kifuani . Kiini cha mauaji hayo bado hakijabainishwa.

Also Read
WHO: Virusi vya Omicron vinasambaa kwa kasi sana

Bamenda ni mji mkuu wa eneo lenye watu wanaozungumza lugha ya kiingereza nchini Cameroon, na ambao unakabiliwa na mzozo wa kisiasa uliosababisha kuzuka kwa makabiliano kati ya makundi ya wapiganaji na maafisa wa kijeshi.

Also Read
Watu wote wazima kuchanjwa dhidi ya covid-19 nchini Marekani
Also Read
Israeli yatangaza hali ya hatari mjini Lod kufuatia mapambano na Palestina

Kulingana na kundi la kimataifa la kushughulikia mizozo ICG, makabiliano hayo yamesababisha kuawa kwa watu 6,000 na zaidi ya wengine milioni moja kuachwa bila makao.

  

Latest posts

ECOWAS kuiwekea Burkina Faso Vikwazo

Tom Mathinji

Rwanda kufungua mpaka baina yake na Uganda

Tom Mathinji

Wakazi wa Kaskazini mwa Ethiopia waghubikwa na baa la njaa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi