Seneta Ron Johnson wa chama wa Republican athibitishwa kuwa na Covid-19

Seneta wa chama cha Republican Ron Johnson amethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Covid-19 lakini yaonekana haonyeshi dalili za ugonjwa huo kwa mujibu wa msemaji wake.

Seneta huyo anayeongoza kamati ya usalama wa ndani na masuaa ya serikali katika seneti,  ataendelea kujitenga hadi atakaposhauriwa na daktari kulingana na msemaji wake.

Also Read
Mshauri wa Trump kuhusu Covid-19 Scott Atlas, ajiuzulu

Hawakueleza jinsi alivyoambukizwa ugonjwa huo.

Johnson ni seneta wa tatu wa chama cha Republican kuthibitishwa kuwa na ugonjwa huo katika kipindi cha siku mbili zilizopita, baada ya Thom Tillis na Mike Lee.

Also Read
Mitch McConnell akosoa wito wa Trump kuhusu msaada kwa waathiriwa wa COVID-19 Marekani

Wengine ni aliyekuwa mshirika wa rais Trump Kellyanne Conway, meneja wa kampeni wa Trump Bill Stepien, mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya chama cha Republican-RNC Ronna McDaniel, na washirika wengine watatu wa ikulu ya White House.

Also Read
Gavana wa benki kuu nchini Sudan Kusini atimuliwa

Haya yanajiri huku Rais wa nchi hiyo Donald Trump akiendelea kutibiwa covid-19 katika hospitali moja ya kijeshi nchini humo

  

Latest posts

Ushirikiano kati ya nchi kubwa na Afrika unatakiwa kuinufaisha Afrika na sio kuwa uwanja wa mivutano

Tom Mathinji

China yawalenga wanafunzi katika kudhibiti Covid-19

Tom Mathinji

Wakazi wote wa Wuhan kupimwa virusi vya Covid-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi