Serikali inajizatiti kuimarisha Viwanda vidogo katika sehemu za mashinani

Serikali inaratibu mkakati maalum ambao utahakikisha kuwa viwanda vidogo vidogo katika maeneo ya mashinani vinatekeleza jukumu muhimu katika kuboresha uchumi wa taifa hili.

Katibu katika wizara ya viwanda Peter Kaberia, amesema kuwa serikali inanuia kuhakikisha kuwa viwanda vidogo vidogo katika maeneo ya mashinani vinaweza kutoa ajira, kuzalisha bidhaa na kuleta teknolojia na huduma nyingine muhimu katika viwango vya mashinani.

Also Read
Kenya Airways na Congo Airways yatia saini mkataba wa ushirikiano

Akiwahutubia wanahabari wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili katika kaunti ya Meru, Kaberia alisema kuwa haya yataafikiwa tu kwa kupeleka rasilmali katika maeneo ya mashinani na kutoa nafasi kwa vijana.

Also Read
Wauguzi wamsihi Rais Kenyatta kusuluhisha mzozo katika sekta ya afya

Alisema kuwa utengenezaji wa bidhaa ambao uko chini ya idara hiyo, ni sehemu ya ajenda nne kuu za rais Uhuru Kenyatta na inapaswa kutekelezwa katika muda wa mwaka mmoja ujao na zaidi.

‚ÄúTunataka kuhakikisha kuwa kuna Viwanda vidogo vidogo katika sehemu za mashinani ambavyo vitatoa ajira na kuleta teknolojia na huduma zingine katika viwango vya mashinani,” alisema Kaberia.

Also Read
Serikali kuanzisha hazina ya kuwarejesha nchini wakenya wanaoteseka ughaibuni

Alisema haya yataafikiwa kwa kupeleka rasilimali katika sehemu za mashinani na fursa za maendeleo kwa vijana ili waweze kushiriki katika ukuaji wa uchumi wa nchi hii.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Mzozo wa kidiplomasia kati ya Uchina na nchi za magharibi wasitishwa

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi