Serikali kujenga jumba la mikutano kwa gharama ya shilingi bilioni 1.4 kaunti ya Kisumu

Serikali imezindua ujenzi wa jumba la mikutano kwa gharama ya shilingi billion 1.4 Jijini Kisumu ili kuwapa nafasi zaidi ya wajumbe 5,000 wakati wa kongamano kuhusu miji mikuu ya Afrika ambalo litaandaliwa Jijini humo mwezi April mwaka ujao.

Waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa amesema jumba hilo ambalo litakuwa la pili la aina yake nchini Kenya, baada ya lile la (KICC) jijini Nairobi litaboresha utalii katika eneo zima la ziwa victoria.

Also Read
Haji akabidhi ripoti ya uchunguzi wa KEMSA kwa Tume ya EACC

Akiongea Jumatatu kwenye uwanja wa maonyesho wa Mamboleo katika kaunti ya  Kisumu wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa jumba hilo, Wamalwa alisema jumba hilo la kifahari ambalo mchoro wake ni kuambatana na utamaduni wa jamii ya wa-Luo, litahudumia Jiji la Kisumu na pia maeneo yaliyo karibu hata baada ya kukamilika kwa kongamano hilo kuhusu miji mikuu ya Afrika.

Also Read
Vijana na wanawake kaunti ya Machakos wanufaika na hazina ya NGAAF

“Jumba hili halitahudumia tu kaunti za maeneo ziwa pekee lakini pia kutokana na ufufuzi wa uchukuzi wa majini, ndugu zetu kutoka Uganda na Tanzania wataandaa mikutano yao hapa,” alisema Wamalwa.

Kwa mujibu wa Waziri huyo wa ugatuzi, serikali inakusudia kutumia fursa ya kongamano hilo kulinyesha ufanisi wa ugatuzi sawia na kutambua fursa za uwekezaji katika eneo hilo la ziwa.

Gavana wa Kaunti ya Kisumu Prof. Peter Anyang Nyong’o alipongeza serikali ya kitaifa kwa kuwekeza katika ujenzi wa jumba hilo.

Also Read
Mshukiwa wa jaribio la mauaji dhidi ya aliyekuwa seneta Kabaka aachiliwa huru

Nyongo alisema jumba hilo la mikutano litawavutia wasafiri wa kibiashara na mikutano kutoka mbali huku Kisumu ikijiandaa kuwa kitovu cha kiuchumi katika Kanda hiyo.

“Hili si swala la kisumu peke yake kwa kuwa litahudumia kaunti zote zilizo Kanda ya eneo la ziwa Victoria,” alisema Gavana huyo wa Kisumu.

  

Latest posts

Rais Ruto: Kenya ina uwezo wa kujiendeleza kiuchumi

Tom Mathinji

Visa 36 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Polisi waimarisha msako dhidi ya Magenge ya wahalifu Magharibi mwa Nchi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi