Serikali kupanda miti katika maeneo yenye vyanzo vya maji

Wizara ya mazingira na misitu imeanzisha mpango kabambe wa upanzi wa  miche katika maeneo yenye  vyanzo vya maji.

Waziri mwandamizi katika wizara hiyo Dkt.Chris Kiptoo alishuhudia kutiwa saini kwa  mkataba wa makubaliano kuhusu jambo hilo kati ya Huduma ya Misitu nchini-KFS na shirika la kitaifa la uhifadhi wa vyanzo vya maji-KTWA,huku akisema ustawishaji wa misitu ni muhimu kwa uhifadhi wa mazingira.

Pande zote mbili zilikubaliana kutumia kipande cha ardhi cha ekari 250 kwenye msitu wa Kaptagat kwa mpango wa majaribio wa kilimo cha mianzi.

Mbegu kutokana na shamba hilo zitagawiwa wakulima katika maeneo chepechepe  huko Nandi,Uasin Gishu,Trans Nzoia na Elgeyo Marakwet ambako hutokea maporomoko ya udongo ya mara kwa mara.

Also Read
Polisi wamkamata mmiliki wa shamba la bangi katika eneo la Soy

Akiongea katika shule ya msingi ya Kaptagat Dkt.Kiptoo alitangaza mpango mkuu wa kurejesha na kuustawisha tena msitu wa Cherengany na eneo la milima  ya Elgeyo ambalo litatangazwa hivi karibuni  kuwa chanzo muhimu  cha maji kwa  mujibu wa arifa iliochapishwa kwenye gazeti rasmi la Serikali.

Also Read
Aliyekuwa Mwakilishi Wadi ya Junju afikishwa mahakamani kufuatia mauaji ya watu watatu Kilifi

Wakatu huo huo wakazi wa kaunti ndogo ya Buuri,kaunti ya Meru wamehimizwa kuhifadhi mazingira kwa kuzingatia upanzi wa miche.

Akiongea alipokuwa akigawa miche kwa wakulima,mwakilishi maalum wa wadi, Joy Karambu aliwataka wakazi wa sehemu hiyo kupanda miche zaidi ili  kuongeza eneo la msitu katika sehemu hiyo.

Karambu alisema sehemu kubwa ya kaunti hiyo ndogo haina msitu,jambo ambalo limesababisha mmomonyoko wa udongo.

Also Read
Serikali yanunu vifaa vya kuondoa gugu-maji katika ziwa Victoria

Alisema hali hiyo isipozuiliwa itasababisha ukame na uhaba wa chakula  katika kaunti hiyo.

Aliongeza kusema kuwa miti ni muhimu kwa kuwa husaidia kuvutia mvua.

Karambu aliwataka wakulima katika sehemu hyo pia kupanda miche kwenye sehemu za mashamba yao ili kuafikia kiwango cha aslimia 10 ya eneo la msitu humu nchini.

Aliwaonya wale wanaoishi kwenye misitu ya serikali  na wale wanaokata miti kiholela kwenye ardhi ya umma kwamba watachukuliwa hatua za kisheria na  ardhi hiyo kutwaliwa na serikali.

  

Latest posts

Mama Taifa ampongeza Jim Nyamu kwa juhudi zake za kuwatunza Ndovu

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 1,335 zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Nyumba za thamani ya shilingi milioni 10 zabomolewa Kitui

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi