Serikali kutambua wauguzi kupitia tuzo za Beyond Zero Health Awards

Serikali imezindua mpango wa kuwatambua wauguzi wanaohudumu katika vituo vya afya ya umma kupitia tuzo za Beyond Zero Health Awards, zitakazofanyika mwezi Septemba mwaka huu.

Akiongea na taifa kupitia mahojiano ya kipekee na radio Taifa, mshirikishi wa tuzo hizo Angella Langat amesema wauguzi wanatekeleza juhudi muhimu wa kuwapa wagonjwa huduma za kimsingi za kiafya; na wakati umefika wa kutambua juhudi zao.    BOFYA HAPA  USIKILIZE  Mahojiano ya Beyond Zero Health    Awards

Angella amesema Beyond Zero Health Awards zinalenga kuwapa wauguzi motisha kazini kama hatua ya kuimarisha huduma za afya kwa mwananchi kupitia mpango unaoongozwa na afisi ya Mama wa Taifa, Margaret Kenyatta. Angella amesema washindi katika tuzo hizo watachaguliwa kupitia mfumo wa kidigitali na hivyo kutakuwa na haki.

Also Read
Rais Kenyatta afungua vituo viwili vya Afya mtaani Kibra
Also Read
Bunge yawaidhinisha mabalozi 14 waliopendekezwa na Rais Uhuru Kenyatta

Angella aliandamana na, Walter Kiptiring, mwenzake kutoka Beyond Zero. Beyond Zero Health Awards zinalenga wauguzi wenye bidii katika vituo vyote vya afya ya umma kuanzia level 2 hadi 5 nchini. Unaweza ukashiriki katika tuzo za Beyond Zero Health Awards kama muuguzi binafsi au kama kundi la wauguzi. Tembelea tovuti www.summit.beyondzero.or.ke kisha chagua application portal ili kujisajili.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi