Serikali kutangaza kafyu Kapedo kati ya saa 12 jioni na saa 12 alfajiri

Serikali inapanga kutangaza sheria ya kutotoka nje usiku katika sehemu ya Kapedo kufuatia visa vya ukosefu wa usalama katika eneo hilo.

Waziri wa Usalama wa Kitaifa Dkt. Fred Matiang’i anasema arifa itachapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali kuwazuia watu kutoka nje kati ya saa kumi na mbili jioni na saa kumi na mbili asubuhi.

Also Read
Oparesheni ya kuwasaka wafungwa 6 waliotoroka gereza la Nanyuki laanzishwa

Kwenye mkutano wa pamoja kati ya Kenya na Uingereza kujadili mabadiliko katika masuala ya usalama duniani na vitisho vya mashambulizi ya kundi la Al-Shabaab, Matiang’i amesema serikali haitasitisha operesheni huko Kapendo, akiongeza kuwa watafanya kila wawezalo kuwapokonya silaha wahalifu.

Also Read
Watu wanane waangamia kwenye makabiliano ya jeshi na wanamgambo wa Al Shabaab mjini Mogadishu

“Miaka michache iliyopita, wahalifu waliua maafisa wetu wa polisi 42, baadaye wakaua maafisa 21 halafu hivi majuzi wakaua maafisa zaidi. Sasa lazima tuwafurushe wote na lazima tuende kukachukue bunduki zote zilizoko,” amesema Dkt. Matiang’i.

Also Read
Wabunge saba wa UDM wajiunga na Kenya Kwanza

Wakati wa mashauriano hayo ya ngazi za juu yaliyoongozwa na Dkt. Matiangi na Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, Ben Wallace, nchi hizi mbili zimekubaliana kuanzisha upya mkataba wa usalama baina yao.

Wallace yuko katika ziara ya siku mbili humu nchini.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi