Serikali kuwasaka wanafunzi ambao hawajajiunga na Kidato cha kwanza

Waziri wa elimu Profesa George Magoha kuanzia Jumatatu juma lijalo atawaongoza maafisa wa wizara yake na wale wa wizara ya usalama wa taifa kwa shughuli ya kuwatafuta  wanafunzi ambao hawajajiunga na shule za sekondari.

Kwenye taarifa, mkurugenzi wa elimu ya shule za sekondari, Paul Kibet, alisema hatua hiyo inadhamiria kuafikia mpito wa asilimia 100 hadi shule za sekondari.

Also Read
Mwenyekiti wa shirika la KBC David Were aifariji familia ya marehemu Justus Murunga

Kibet aliongeza kusema kwamba wakati wa shughuli hiyo wizara ya elimu itawafahamisha Wakenya jinsi wanafunzi wanavyojisajili katika kidato cha kwanza kote nchini, akisema serikali itahakikisha wanafunzi wote waliofuzu wanajiunga na kidato cha kwanza cha shule ya kutwa ya sekondari iliyoko karibu.

Also Read
Wanafunzi 441 waliofanya KCSE mwaka 2021 kukosa matokeo yao

Kulingana na katibu huyo wa elimu, shule za upili za kutwa hazitozwi karo yoyote, kwa hivyo wazazi ambao hawajimudu wanapaswa kuwapeleka watoto wao katika shule hizo za kutwa.

Also Read
Kipruto asema yuko shwari kisaikolojia kutetea taji yake ya dunia

Alisema kaunti nyingi kati ya kaunti 47 zimekuwa na usajili wa kuridhisha wa wanafunzi wanaojiunga na kidao cha kwanza baada ya kukamilika muda wa wanafunzi kufika shuleni wiki moja iliyopita.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi