Serikali ya Kaunti ya Embu yawarejesha kazini wafanyikazi 1,200 wa Afya

Serikali ya kaunti ya Embu imewarejesha kazini wafanyikazi vibarua 1,200 wa sekta ya afya, baada ya wenzao wanaohudumu kwa masharti ya kudumu kutishia kuendelea na mgomo wao. 

Wafanyikazi hao wamekuwa mgomoni kwa wiki mbili sasa kuhusu malimbikizi ya mishahara na walikuwa wamekubali kutia saini mkataba kuhusu masharti ya kurejea kazini.

Also Read
Wahudumu wa afya wa kujitolea kaunti ya Embu watishia kusitisha huduma zao

Hata hivyo wanasema wataweza tu kutia saini mkataba huo baada ya wenzao vibarua kurejeshwa kazini.

Also Read
Serikali kuwasaka majangili katika kaunti ya Laikipia

Kwenye barua ya tarehe 15 Septemba mwaka huu, utawala huyo wa kaunti ulikuwa umewafuta kazi wafanyikazi wote vibarua kwa “kukosa kufika kazini bila idhini.”

Barua ya kusimamishwa kwao ilitiwa saini na katibu wa kaunti hiyo Johnson Nyaga.

Also Read
Washukiwa wa mauaji ya kaka wawili wa Kianjokoma wataka miili hiyo ifukuliwe

Hata hivyo, mwenyekiti wa chama cha kitaifa cha wauguzi Joseph Ngwasi amesema hakuna mfanyikazi yeyote atakayerejea kazini pasipo wenzao vibarua kurejeshwa kazini.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi