Serikali ya Kaunti ya Samburu yadaiwa kutumia shilingi milioni 147 kwa miradi ghushi

Serikali ya Kaunti ya Samburu huenda ilitumia shilingi milioni 147 kulipia bili za miradi gushi wakati wa kipindi cha matumizi ya pesa za serikali cha mwaka 2018 /2019.

Kwa muijibu wa ripoti mpya kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa serikali Nancy Gathungu, kaunti hiyo inadaiwa kuwa ililipa fedha hizo kwa Wizara za Maji, Mazingira na Kawi.

Also Read
Kenya yapokea chanjo 180,000 za Astrazeneca kutoka Ugiriki

Kulingana na ripoti hiyo iliyowasilishwa kwenye Bunge la Seneti, Kaunti ya Samburu ilitoa malipo ya shilingi milioni 127.8 kwa Wizara ya Maji na shilingi milioni 19.88 kwa Wizara ya Kawi.

Also Read
Mahakama Kuu yazuia kwa muda kufurushwa kwa Seneta Isaac Mwaura

Hata hivyo, bili hizo hazionekani popote kwenye taarifa za kifedha za kaunti hiyo huku stakabadhi husika zikikosa kutolewa na hivyo kuibua wasi wasi kwamba huenda fedha hizo zilitumika kwa miradi isiyokuwepo.

Also Read
Mutyambai aamuru uchunguzi kuhusu ghasia za Murang’a

Kumekuwa na wasi wasi kwamba kaunti nyingi na pia taasisi za serikali zinatumia billi gushi kama njia za kufuja fedha za umma.

  

Latest posts

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Kagwe: Watoto hawatachanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi