Serikali ya Kenya yajibu madai ya Somalia kwamba ilishawishi ripoti ya IGAD

Serikali imejibu madai ya Somalia kuhusu ripoti ya Shirika la IGAD iliyoiondoa Kenya lawamani kuhusiana na dhana ya kuingilia masuala ya ndani ya taifa hilo jirani.

Katika taarifa yake siku ya Jumatano, Somalia ilidai kuwa ripoti hiyo ina mapendeleo na ilishawishiwa ili kuiondoa Kenya lawamani.

Also Read
Junet aomba msamaha kwa kumdhalilisha Seneta Mwaura kwa misingi ya ulemavu

Hata hivyo, Wizara ya masuala ya kigeni humu nchini ilisifia ripoti hiyo ya IGAD ikisema imeiondoa Kenya lawamani kuhusiana na mzozo wa kidiplomasia na Somalia na kudhihirisha kuwa madai ya Somalia dhidi ya Kenya hayana msingi.

Also Read
Wazazi Garissa wataka shule zifungwe kufuatia ongezeko la visa vya Covid-19

Somalia ilikuwa imeshutumu Kenya kwa kuingilia masuala yake ya ndani, madai ambayo Kenya ilikanusha.

Hata hivyo, hatibu wa serikali, Kanali Mstaafu Cyrus Oguna, amethibitisha kuwa madai ya Somalia hayakuwa na msingi wowote.

Also Read
Wakulima wa pamba Lamu waiomba serikali kuwapa ruzuku ya pembejeo ili kuimarisha faida

Oguna amekariri kuwa haiwezekani kwa Kenya kuvuruga udhabiti wa Somalia ilihali wanajehsi wake wanahudumu kwenye kikosi cha AMISOM kinacholinda amani nchini Somalia.

Kundi la IGAD lililochunguza madai hayo liliongozwa na Rais wa Djibouti, Ismali Omar Guelleh.

  

Latest posts

Wakazi wa Nandi ya kati wahimizwa kushirikiana na polisi kukabiliana na uhalifu

Tom Mathinji

Serikali yahimizwa kutoa mikopo ya HELB kwa wanafunzi wa vyuo vya kibinafsi

Tom Mathinji

Mahakama iko tayari kwa kesi za uchaguzi mkuu ujao asema Jaji mkuu Martha Koome

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi