Serikali ya Sudan yatia saini mkataba wa Amani na viongozi wa Waasi

Serikali ya Sudan na viongozi wa waasi wametia saini mkataba wa kihistoria wa amani unaolenga kukomesha vita vilivyodumu kwa miongo mingi ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu.

Mkataba huo wa amani uliotiwa saini leo jijini Juba nchini Sudan kusini ulipatanishwa na nchi kadhaa zikiwemo Kenya, misri na Sudan kusini.

Also Read
Kampeni za uchaguzi mdogo wa useneta wa Machakos zasitishwa

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka aliyeakilisha Kenya alisema kuwa mikataba ya amani inahitaji kujitolea ili itekelezwe.

Alisema kuwa wakati umewadia kwa bara Afrika kukomesha vita na kuungana ili kuliendelea bara hili.

Katibu mkuu mwandamizi katika wizara ya mashauri ya nchi za kigeni Ababu Namwamba alisema kuwa amani katika eneo hili italeta ukuaji na maendeleo.

Also Read
Agnes Kavindu aapishwa kuwa Seneta wa Machakos

Rais Salva Kiir  wa Sudan kusini alisema kuwa uthabiti nchini Sudan utanufaisha nchi yake pia.

Makundi saba ya waasi kutoka Darfur na Sudan magharibi yalisema yatasitisha vita na kuleta umoja kwenye mkataba wa amani uliopatanishwa na serikali za kanda hii.

Also Read
Zaidi ya watu 100 wafariki kutokana na mafuriko nchini Sudan

Kukomeshwa mizozo ya ndani nchini Sudan kumepewa umuhimu na serikali ya mpito nchini humo iliyotwaa mamlaka mara tubaada ya kung’atuliwa kwa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir. Mkataba huo wa amani nchini Sudan umesifiwa na viongozi mbalimbali duniani kuwa wenye manufaa kwa umoja ulimwenguni.

 

  

Latest posts

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Ethiopia yakaribisha wito wa kurejelewa mazungumzo na majirani wake kuhusu bwawa katika mto Nile

Tom Mathinji

Bwawa katika mto Nile lazidisha uhasama kati ya Ethiopia, Sudan na Misri

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi